*DEREVE WA LORI LA MAJI APEWA KIPONDO KISA KUANZA YEYE KUINGIA NJIA NDOGO

 Dereva wa Loro la Maji wa Kampuni ya Dolfin yenye maskani yake Mbezi Tang Bovu, jijini Dar es Salaam,ambaye hakuweza kufahamika jina lake mapema, akiugulia maumivu baada ya kupigwa na kuumizwa na jamaa wawili waliokuwa na kina dada wawili katika gari ndogo eneo la Mbezi njia inayoingia katika Shule ya Mbezi Beach Sekondari jana usiku. 

Dereva huyu alikuwa akitokea Barabara kubwa akiingia katika njia ndogo inayoelekea Shule ya Sekondari ya Mbezi Beach, na gari ndogo ilikuwa ikitokea katika njia hiyo ndogo na kukutana uso kwa uso na lori hilo, huku watu waliokuwa katika gari hiyo ndogo wakimtaka dereva wa lori kuwapisha wao ili waanze kupita. 

Dereva huyu aliamua kubana kushoto na kuwaachia njia ili wapite, kama picha ya Lori inavyoonyesha chini, laiki jamaa waliokuwa katika gari ndogo waliamua kushuka na kumshusha dereva huyo na kisha kuanza kumshambulia kwa magumi na mawe, huku dereva huyo akitoka nduki na kuacha gari lake, hadi katikati ya barabara inayoelekea Tegeta ikitokea Mwenge, walipomtia mikonini na kuanza kumpiga kama mwizi huku wakitumia mawe kumpigia kama makwenzi, na kumuumiza kama hivi, hadi walipofika watu kibao na kuanza kuamulizia ugomvi huku wakijua kuwa jamaa huyo ni mwizi huku wengine wakijandaa kunza kumshambulia. 

Lakini watu hao baada ya kupata stoti kamili ilivyokuwa waliamua kuwageuzia kibao watu hao wakianza kuwasonga kutaka kuwashambulia ndipo walipoamua kudandia gari na kukimbia, huku mmoja kati ya wanawake waliokuwa na jamaa hao, akisikika kumwambia jamaa huyo,

''usirudie kutukana watu waliovaa suti hovyo bila kuwajua watakuua''. 

Gari hiyo wakati ikianza kuondoka eneo hilo hukuikiendeshwa na mwanamama, ilianza kushambuliwa kwa mawe kwa bahati iliwahi kuondoka eneo hilo na kuingia usawa wa Barabara ya Masana na kutokomea.
 Watu hao wakidandia gari iliyoanza kutembea ili kutoweka eneo hilo.
 Jamaa hao wakianza kuondoka eneo hilo kwa kasi huku gari hiyo ikiendeshwa na Mwanamama.
 Lori lililozua kasheshe hilo, ndiyo hili na eneo lenyewe ndo kama hivi linavyoonekana huku magari yakiwa na uwezo wa kupita bila kugusana na lori hilo.
Lori hilo likiwa limeachwa katika eneo la tukio baada ya dereva wake kupewa kipondo huku magari mengine yakipita kama kawaida.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.