*ET'OO KUWAONGOZA WENZAKE 20 KUTUA DAR KUIKABILI STARS


MCHEZAJI wa Kimataifa, Samue Et'oo, ni mmoja kati ya wachezaji 21 waliotajwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Cameroon (FECAFOOT) kuwa katika msafara wa watu 36 wakiwemo viongozi wa timu yao ya Taifa 'Indomitable Lions' wakiongozwa na nahodha huyo Samuel Et’oo Fils kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumatano.
Kiongozi wa msafara wa timu hiyo itakayoanza kuingia nchini keshokutwa (Februari 3 mwaka huu) ni Mwakilishi wa Serikali ya Cameroon, Dieudone Wassi. Naibu kiongozi wa msafara wa Cameroon itakayofikia hoteli ya New Africa ni Makamu wa Rais wa FECAFOOT, John Ndeh.
Mbali ya Et’oo, wachezaji wengine waliomo kwenye msafara huo ni Charles Itandje, Benoit Assou Ekoto, Jehu Rustand Youthe (Union Douala), Fabrice Olinga Essono, Allam Nyam, Bouba Aminou, Benoit Angwa, Herve Tchami, Henri Bedimo, Nicolas Nkoulou, Jean Makoun, Jean Kana Biyick, Joel Matip, Vincent Aboubakar, Alexandre Song, landre Nguemo, Pierre Wome, Jean Nyontcha, Achille Emana na Charles Eloundou.
Wengine ni Andre Nguidljol Nlend (Mkurugenzi wa Utawala FECAFOOT), Jean Paul Akono (Kocha Mkuu), Martin Ndtouungou Mpile (Kocha Msaidizi), Jacque Songo’O (Kocha wa makipa), Dk. Baoubakary Sidiki (Daktari wa Timu) na Emmanuel Francis Ambane (Psychologist).
Pia wapo Tchonkontey Monkam (Fitness Trainer), Rigobert Song (Meneja wa Timu), Aoudou Mvotoung (Team Security), Fouda pascal Linus (Ofisa Habari FECAFOOT), Boubakar Ndou (Meneja Vifaa), Daniel Tcheuffa Tecky (Physiotherapist), Elias Kalaguem (Physiotherapist) na Justin Addo (Wakala wa Mechi).
Wakati huo huo, kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini kesho jioni (Februari 2 mwaka huu) kwenye hoteli ya Tansoma.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA