Ni hali halisi ndani ya Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera  usiku wa kuamkia leo.
 Kwa mujibu wa taarifa zilizo naswa toka kwa wafanyakazi wa Meli hiyo ambao hawakutoa ushirikiano kuzungumza na waandishi wa habari, zilizonaswa wakati wakilaumiana zimeleeza kuwa mafundi wa kampuni hiyo walikuwa wakichomelea katika moja ya vyumba vya chini vya Meli hiyo ndipo cheche za moto zilipopenya na kuangukia katika sehemu ya pili ya kuhifadhia mizigo na kuanza kuwaka. Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa shehena ya magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera usiku wa kuamkia leo.
Maafisa wa kikosi hicho walijitosa kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria ambapo walifanikiwa kuuzima huku ukiwa tayari umeteketeza magodoro yote pamoja na mito ya makochi iliyokuwa katika chumba cha kuhifadhia mizigo.
 MELI ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini (MSC) imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo wakichomelea eneo la shimo la kuhifadhia mizigo la mojawapo ya maeneo kwenye Meli hiyo. Moto huo uliozuka katika meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji la Mwanza na kufurika katika eneo la maegesho ya Meli za Kampuni ya MSC yaliyopo katika bandari ya Mwanza kaskazini majira ya saa 8 na dakika kadhaa na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo.
 Saa 3 na dakika 10 meli ya Mv. Victoria inaondoka Mwanza.... kuelekea Bukoba mkoani Kagera.
 Mv Victoria ikijitayarisha kwa ajiri ya kufanya safari yake usiku wa leo kuelekea mjini Bukoba mkoani Kagera mara baada ya kukaguliwa kufuatia kunusurika kuteketea mchana wa leo kupitia sakata la wachomeleaji walio sababisha moto uliozuka eneo la kuhifadhi mizigo.
 Mv. Victoria ikipakia gari usiku huu hatimaye kuanza safari yake usiku huu.
 Nao wasafiri walipanda kama ada licha ya baadhi yao kuonekana kuwa na wasiwasi na wengine kuahirisha kabisa safari.
Ndani ya meli abiria wakitathimini mazingira.Picha zote na Mdau Gsengo-Clouds FM

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.