Flaviana aendelea kuula Majuu


Na Mwandishi wetu
Mwanamitindo wa kimataifa kutoka nchini Tanzania Flaviana Matata ameshiriki katika kampeni za matangazo makubwa ya makampuni ya nguo ya Diesel na  Edun.
 Kampeni hiyo inayoitwa Diesel + Edun ilianzishwa mwaka jana mwezi wa kwanza ambapo muanzilishi wa kampuni hiyo, Renzo Rosso - na waanzalishi wa kampuni ya Edun ,  Ali Hewson na Bono walisafiri nchi za Uganda na Mali na kukutana na wakulima wa pamba barani Afrika.
Waanzilishi hao waliingia makubaliano ya kutengeneza nguo maalum zitakazotokana na pamba ya wakulima hawa wa Afrika na hivyo kuwanufaisha moja kwa moja. Hivyo basi nguo hizi zinatangazwa kama kampeni ili kunufaisha bara la Afrika.
Nguo hizo zitaanza kupatikana mwanzoni mwa mwezi wa tatu katika maduka mbalimbali nchini Marekani na duniani. Pia nguo za Diesel + Edun zitauzwa kupitia mitandao mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Compass Communications Limited, Maria Sarungi Tsehai amesema kuwa Flaviana ambaye aliwahi kuwa Miss Universe Tanzania 2007 anabaki kuwa mwanamitindo pekee kutoka bara la Africa katika kushiriki katika kampeni za nguo hizo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU