IBF YACHUKUA NAFASI YA KATIKATI BARANI AFRIKA.

ZOEZI la upimaji uzito katika mapambano mawili ya IBF yanayofanyika katika majiji ya Johannesburg na Tunis lilifanyika vizuri jana.
Mapambano hayo yamepewa jina la “Barabara ya kutoka Cape Town mpaka Cairo kwa IBF” kutokana na majiji haya kukaa moja kusini na lingine kaskazini mwa Afrika, yanafanyika wakati IBF ikijipambanua vyema katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi.
Kusini mwa Afrika, leo imeshughudia mabaondia mawili wanaopambania ubingwa wa dunia kwa vijana walio chini ya miaka 25 wakipima uzito mbele ya mashirika mbalimbali ya habari ya ndani na nje ya Afrika ya Kusini.
Illunga Makabu kutoka Jamhuri ay Watu wa Kongo (DRC) alipima uzito kumkabili Gogota Gorgiladze wa Georgia. Upimaji huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa ulio katika hotel ya nyota tano ya Emperors Palace iliyoko katika jiji la Johannesburg!
Rodney Berman mtu anayeheshimika kwa kuwa promota wa kwanza kuandaa pambano la IBF la dunia katika bara la Afrika mwaka 1990, ndiye anayepromoti pambano hili!
Tayari wadau na mashabiki wa ngumi kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika zikiwamo Namibia, Zambia, Msumbiji, Zimbabwe na Tanzania wameshawasili nchini Afrika ya Kusini tayari kuangalia mpambano huo. Wengine walibaki Afrika ya Kusini wakati wa mashindano ya kombe la Afrika yaliyomalizika wiki iliyoita.
Msimamazi mkuu wa mpambano huu ni Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi aliyesimama pichani na mabondia Gogita Gorgiladze (kushoto) na Ilunga Makabu (kulia)
 
Kaskazini mwa Afrika,
Bondia ambaye ameshajizolea sifa kemkem Ayoub Nefzi wa Tunisia anayeishi nchini Belgium atapigana na bondia Ishmael Tetteh kutoka nchi ya Ghana kugombea ubingwa wa Afrika, Ghuba ya Uajemi  na Mashariki ya Kati (IBF AMEPG) katika uzito wa Light Middle.
Mpambano huo uliopewa jina la “Uzuri wa Jasmine” kutokana na jina hilo kutumika katika mapinduzi yaliyomwondoa Rais wa zamani wa Tunisia Ben Ali unafanyika wakati Ayoub Nefzi akijiandaa kugombea mkanda wa juu wa IBF wa mabara mwezi wa tatu nchini Belgium.
Mabondia wote wawili wanatagemea kuonyesha moto mkali katika mpambano ambao tayari mashabiki wa ngumi kutoka katika nchi za Nigeria, Ghana, Libya, Misri, Algeria tayari wameshawasili nchini Tunisia kuangalia mpambano huo!
Tunisia inasifika kama nchi iliyowahi kutoa viongozi wengi wa mchezo wa ngumi katika bara la Afrika.
 Imetolewa na:
 INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*