MAMA SALMA KIKWETE ATOA MSAADA WA VIFAA VYA HOSPITALI YA SOKOINE - LINDI

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akimshika kwa furaha mtoto aliyezaliwa tarehe 5.7.2013 katika hospitali ya Mkoa wa Lindi, Sokoine huku mama wa mtoto huyo Muksim Issa ,19, anayetoka katika kijiji cha Mumbu kilichoko katika wilaya ya Lindi vijijini aliyelala kitandani akitabasamu. Mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa kilo 3.9  Mama Salma alitembelea hospitalini hapo kukabidhi vifaa vya hospitali tarehe 6.2.2013. Aliyesimama kulia kwa Mama Salma ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dr. Nasoro Hamid. PICHA ZOTE/JOHN LUKUWI


Kikundi cha utamaduni kikiwatumbuiza waalikwa kwa ngoma ya Tambiko inayochezwa na watu wa kabila la Wamakonde wakati wa  sherehe ya kukabidhi vifaa vya tiba kwenye hospitali kuu ya mkoa wa Lindi, Sokoine, tarehe 6.2.2013.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi kwa vifaa vya hospitali ya mkoa wa Lindi,Sokoine, vilivyotolewa na Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Shirika la Project C.U.R.E. la nchini Marekani. Vifaa hivyo vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia saba. Kulia kwa Mama Salma ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Dr. Nasoro Hamidi akifuatiwa na Katibu wa CCM WA Mkoa huo Ndugu Adelina Gefi na kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali Dr. Nicolaus Munni.  Sherehe hiyo ilifanyika tarehe 6.2.2013.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete kwa furaha akiagana na wafanyakazi wa hospitali ya Mkoa wa Lindi,Sokoine, viongozi na wananchi waliohudhuria sharehe za kukabidhi vifaa vya hospitali hiyo tarehe 6.2.2013.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI