MAMA SALMA: RAIS KIKWETE ANA HASIRA, WANAOSEMA MPOLE HAWAMJUI

*UCHESHI WAKE NI HAIBA TU
*HUKASIRIKA ANAPOONA MTENDAJI WA HOVYO AU MZEMBE
MAMA SALMA KIKWETE
NA BASHIR NKOROMO, LINDI
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCN, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoboa siri kwamba mumewe, Rais Jakaya Kikwete pamoja sura yake kujawa na haiba ya ucheshi wa mara kwa mara lakini kwa tabia ana hasira.

Amesema, Rais Kikwete hukasirika sana hasa anapoona au kusikia mtu au mtendaji katika Chama au serikali anafanya mambo ya hovyo au ya kizembe hasa katika masuala ya kazi.

Mama Salma Kikwete ametoboa siri hiyo, leo Februari 18, 2013, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kikwetu Kata ya Mbanja akiwa katika ziara ya kukagua, kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na kuwashukuru wana-CCM wa Lindi mjini kwa kumchagua kuwa mjumbe wao wa NEC.

"Siyo kweli kwamba Rais Jakaya Kikwete siyo mkali, japokuwa ana sura yenye haiba ya ucheshi wa mara kwa mara kwa kila mtu, lakini ana hasira, tena  sana pale mtendaji au mtu yeyote anapombaini kwamba anafanya mambo ya hovyo au kizembe katika kazi za Chama au serikali yake", alisema Mama Salma Kikwete.

Mama Kikwete akitoa ufafanuzi, baada ya mshereheshaji mmoja kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Lindi mjini Muhsin Ismail, kusema kwamba Rais Jakaya Kikwete ni mpole wa kupindukia na kuuliza umati wa wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo kwamba je ni nani amewahi kumuona amenuna.

"Natoa ofa kama hapa kuna mtu aliyewahi kumuona mpendwa wetu, Rais Kikwete amenuna anyooshe mkono. Akitokea ntampa sh. elfu moja hapa hapa... Kwa mara ya akwanza, ya pili unaona hakuna", alisema Muhsini.

Wakati akiendelea kusema hivyo, mtu mmoja kwenye mkutano huo alinyoosha mkono, lakini Muhsin akakataa kumpa zawadi yake kama alivyokuwa ameahidi. "Aaa wewe sikupi zawadi", alisema Muhsini lakini papo hapo akakatishwa na Mama Mama Kikwete.

"Hata kama humpi hiyo zawadi, sawa. lakini Siyo kweli kwamba Rais Jakaya Kikwete hakasiriki na siyo mkali. Japokuwa ana sura yenye haiba ya ucheshi wa mara kwa mara kwa kila mtu, lakini ni ana hasira, tena  sana pale mtendaji au mtu yeyote anapombaini kwamba anafanya mambo ya hovyo ay ya kizembe..." alisema Mama Kikwete.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*