Matumaini kurejea hospitali baada ya kumaliza dozi

 

Na Elizabeth John
MUIGIZAJI wa filamu za kibongo na mchekashaji, Tumain Martin ‘Matumaini’ anatarajia kurudi hospitali ya Amana jiijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza dozi ya dawa alizopewa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, rafiki wa karibu wa msanii huyo, Robart Kiwewe ‘Kiwewe’ alisema kuwa Matumaini alikaa hospitalini hapo kwa muda wa siku tatu akiwa anasumbuliwa na miguu ambapo jana aliruhusiwa kurudi nyumbani.
“Hivi nimetoka nyumbani kwao Yombo kumuangalia bado hali yake nsio nzuri, daktari kampa dawa kamwambia arudi hospitali baada ya kumaliza kumeza dawa hizo, Watanzania tunatakiwa kumuombea mwenzetu ili arudi katika hali yake ya kawaida,” alisema Kiwewe.
Alisema hali yake sio nzuri kwani hadi sasa hajui ni ugonjwa gani unaomsumbua, taarifa walizozipata mwanzo ni kwamba alianza kusumbiliwa miguu ikafuata na mikono na sasa maumivu yamesambaa sehemu mbalimbali za mwili wake, kutokana na kushindwa kugundua ugonjwa unaomsumbua daktari ameamua kumpa dawa za kupunguza maumivu.
Kiwewe alisema kwasasa hawana utaratibu mwingine ambao wameweza kuufanya mpaka amalize kumeza dawa hizo na kurejea tena hospitali.
Matumaini alikwenda kuishi nchini Msumbiji na kulipotiwa kusumbuliwa na maradhi lakini alishindwa kutibiwa akiwa huko ambapo Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla alichukua jukumu la kumpatia nauli ya kumrudisha nchini.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI