MESSI, KAPOMBE KUJARIBU BAHATI SUNDERLAND YA ENGLAND

Alhaj Rage

Na Dina Ismail
WACHEZAJI chipukizi wa timu ya soka ya Simba Ramadhan Singano ‘Messi’ na Shomari Kapombe wanatarajiwa kwenda kufanya majaribio katika kituo maalum cha vijana cha klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya England, Sunderland.
Aidha, vuiongozi wa Simba, wanatarajiwa kwenda huko hivi karibuni  ambapo pamoja na mambo mengine watashuhudia mechi ya ligi kuu ya England baina ya wenyeji Sunderland dhidi ya Fulham itakayopigwa Machi 2 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage alisema, hatua hiyo inafuatia ushirikiano baina yao na Sunderland uliotokana na matunda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
Alisema katika makubaliano yao ya ushirikiano na udhamini, Sunderland ambayo imepania zaidi kuwekeza katika soka la vijana ambapo itakuwa ikichukua wachezaji katika makundi tofauti ya umri wa klabu ya Simba na kwenda kujifunza katika taasisi yao ya vijana.
Rage aliongeza kuwa, Kapombe na Singano watakwenda huko mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Vodacom ambapo pamoja na kupatiwa mafunzo maalum katika kituo cha kulea vijana cha timu hiyo, kama watafanya vema katika mazoezi yao huenda wakasajiliwa kuichezea timu ya vijana ya Sunderland.
Aidha, Rage aliongeza kuwa mazungumzo kuhusiana na udhamini wao na Sunderland yapo katika hali na ndiyo maana uongozi umealikwa kwenda huko si kwa ajili tu ya kushuhudia mechi bali kubadiklishana uzoefu na viongozi wa timu hiyo.
Akizungumzia maandalizi ya mechi yao yao ya ligi ya mabingwa Afrika kesho dhidi ya CR Libolo ya Angola, Rage alisema kikosi cha timu hiyo kipo katika hali nzuri na wachezaji wana ari kubwa ya kuhakisha wanashinda, hivyo amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuishangilia.
Kuhusiana na kusuasua kwa Simba kwenye ligi kuu bara, Rage alisema hiyo inatokana na timu zote zinazoshiriki ligi hiyo kujipanga vema,huku akibeza watu wanaoendekeza ushabiki zaidi badala ya kuangalia ushindani uliopo uwanjani.
Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Simba, Rahma Al Kharoos amewataka watu kujitokeza kwa wingi kuishangilia Simba katika mchezo wake wa kesho huku akiwasihi zaidi wanawake wenzake kwenda kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam utakapopigwa mchezo huo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.