Peter Kenneth
Peter Kenneth alizaliwa tarehe
27 Novemba mwaka 1965 na anatoka mkoa wa kati. Ndiye mgombea wa kwanza
asiye na jina asilia la kiafrika.
Akiwa ndiye mgombea mwenye umri mdogo sana,
anasisitiza kuwa , yeye kama kiongozi mwenye mchanganyiko wa makabila,
atahakikisha kuwa ukabila ambalo ni tatizo sugu Kenya , unamalizika.Kama naibu waziri, katika serikali ya Rais Kibaki,Kenneth anagombea urais kwa muungano wa EAGLE, ambao umewaleta pamoja waliokuwa wanafunzi wenza katika shule ya sekondari ya Starehe . Mgombea mwenza wa Peter Kenneth ni meneja mkuu katika kampuni ya huduma za simu ya Safaricom.
Kenneth alikuwa mgombea wa kwanza wa urais kuzindua ruwaza yake ambayo ilitaja sekta 13 ambazo atazipatia kipaombele ikiwa atashinda urais.
Ni pamoja na kuhakikisha uwepo wa chakula, kushughulikia swala la ukosefu wa ajira, kuimarisha huduma za afya, elimu, utalii , kilimo, maji , kudhughulikia maswala ya wakenya wanaoishi ughaibuni, viwanda na uzalishaji wa bidhaa.
Anasema kuwa ananuia kuongeza uzalishaji wa chakula, kwa kutengeza miradi kumi ya unyunyiziaji maji mashamba. Pia anaahidi kuwa serikali yake itapunguza bei ya mazoa ya kilimo pamoja na kuondoa kodi ka mazao ya shambani.
Comments