Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akiwa amembeba mtoto wa kiume aliyezaliwa jana saa 11 alfajiri (Februari 7, 2013) na Bi. Fatma Mohammed kwenye kituo cha afya cha Kijiji cha Matumaini. Mama wa mtoto huyo, Bi. Fatma Mohammed alisema atamwita mtoto huyo Pinda kwa sababu Mama Pinda amekuwa mtu wa kwanza kumjulia hali.
  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (kulia) akiwa amembeba mtoto Elizabeth (mwenye miezi saba) anayelelewa katika kituo cha afya cha Kijiji cha Matumaini wakati alipotembelea kijiji hicho Februari 7, 2013.
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (kulia) akiwa amembeba mtoto Elizabeth (mwenye miezi saba) anayelelewa katika kituo cha afya cha Kijiji cha Matumaini wakati alipotembelea kijiji hicho Februari 7, 2013.
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (kulia) akiwa amembeba mtoto Cyprian (doto) mmojawapo wa mapacha wanaolelewa katika kituo cha afya cha Kijiji cha Matumaini wakati alipotembelea kijiji hicho Februari 7, 2013. Pacha mwingine (kulwa) Christian)  amebebwa na Mwenyekiti wa UWT, Mkoa wa Dodoma, Bi Salome Kiwaya.  Kushoto ni Pd. Vincent Boselli akielezea jinsi watoto hao wenye miezi mitatu walivyofikishwa kituoni hapo wakitokea Morogoro.
Neema Ntandu (wa tatu kushoto) ambaye ni mmojawapo wa watoto watatu waliokuwepo wakati Kijiji cha Matumaini kikianzishwa mwaka 2002, akimkabidhi zawadi ya sanamu ya Bikira Maria, Mama Tunu Pinda ambayo imetengenezwa na watoto wa kijiji hicho wakati Mama Pinda alipotembelea kijiji hicho jana mchana, Februari 7, 2013. 
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (wa pili kulia) akiwa amembeba mtoto Consolatha kwenye shule ya awali ya Kijiji cha Matumaini kinacholea watoto yatima eneo la Kisasa, Dodoma jana mchana Februari 7, 2013. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT, wilaya ya Dodoma Mjini, Bi. Fatuma Mwenda na (kushoto) ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa huo, Bi Salome Kiwaya.
Baadhi ya watoto wa Kijiji cha Matumaini wakiangalia zawadi walizopelekewa jana  Februari 7, 2013 na Mama Tunu Pinda wakati alipotembelea kijiji hicho. Picha na Irene Bwire –Ofisi ya Waziri Mkuu

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA