MKURUGENZI MKUU WA ELIMU AACHIA MANYANGA

Na Beatrice Shayo

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania, Dk Paul Mushi. Kufuatia sakata kuwa Serikali haina mitaala rasmi ya kufundishia shuleni, Mkurugenzi  Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania, Dk Paul  Mushi (pichani),  amejiuzulu wadhifa huo. Nafasi yake imechukuliwa na  Mkurugenzi wa Idara ya kubuni  na kuendeleza Vifaa vya Elimu, Dk. Leonard Akwilapo.
 
Akihojiwa na  NIPASHE kwa njia ya simu jana jijini Dar es Salaam,  Dk. Mushi alithibitisha kujiuzulu na kusema alichukua hatua hiyo kwa hiari yake   bila kushinikizwa na mtu.
 
"Hakuna aliyenishinikiza nimeamua mwenyewe kuandika barua ya kujiuzulu," alisema Dk. Mushi
 
Kwa upande wake,  Kaimu Mkurugenzi Dk. Akwilapo alipohojiwa juu ya mtangulizi wake   aliyeachia ngazi , Alhamisi wiki hii, alisema aliondoka kwa maamuzi yake mwenyewe bila shinikizo kama alivyoeleza.
"Sio siri ni kweli amejiuzulu na aliniambia ni maamuzi yake aliyoyafanya ya kujivua madaraka ya Mkurugenzi Mkuu bila ya kugombana na mtu na juzi ndio alipewa barua yake na mimi kupatiwa barua ya kuwa kaimu," alisema Dk Akwilapo
 
Katika mkutano wa  Bunge la mwezi huu, Mbunge wa kuteuliwa na Rais  James Mbatia (NCCR-Mageuzi),  aliwasilisha bungeni hoja binafsi kuhusu udhaifu uliopo katika sekta ya elimu hapa nchini.
 
Katika hoja hiyo, aliibua sakata la kutokuwapo kwa  mitaala inayoongoza ufundishaji wa masomo shuleni hali inayosababisha kudorora kwa elimu.
 
Kadhalika  aliibua tuhuma za uchapishwaji wa vitabu ambavyo maudhui  yake hayana viwango pia waliopewa kazi ya kuchapisha ndiyo hao waliokuwa wahariri na waandishi .
 
 Pia alihoji sababu za uchapishaji wa vitabu hivyo  kufanyika nje  ya Tanzania hali ambayo inasababisha kuwapo kwa matumizi mabaya ya fedha .
 
Katika kujibu hoja hizo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi alilithibitishia Bunge kuwa serikali ina mitaala na nakala zake ziliwasilishwa bungeni  na hoja hiyo ikazimwa.
 
Baada ya kuwasilishwa kwa mitaala hiyo, bunge iliunda kamati ya kujiridhisha kama ni kweli mitaala hiyo ni sahihi ambapo ilikuja na majibu ya kujiridhisha kuwa ni ya kweli.
 
Hata hivyo, kwa upande wa James Mbatia alisema bado kuna utata katika mitaala hiyo licha ya kamati hiyo kujiridhisha kuwa mitaala ipo sahihi.
CHANZO: NIPASHE

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA