NGASSA NA BOBAN HAWAJASIMAMISHWA SIMBA SC, ILA...

Mrisho Ngassa

Na Mahmoud Zubeiry
WACHEZAJI wawili tegemeo wa Simba SC, Mrisho Khalfan Ngassa na Haruna Moshi Shaaban, watakuwa na kikao leo saa 5:00 na uongozi wa Simba, kufuatia kesi iliyowasilishwa dhidi yao kwa uongozi na Kocha Mfaransa, Patrick Liewig.
Habari za uhakika, kutoka ndani ya Simba SC, zimesema kwamba, Liewig amewasilisha malalamiko ya kinidhamu dhidi ya wachezaji hao na kuomba uongozi ukutane na wachezaji hao kuzungumza nao, ili wabadilike.
BIN ZUBEIRY inafahamu Simba SC haiko tayari kuwachukuliwa hatua zozote kali wachezaji hao kwa wakati huu, zaidi ya kuzungumza nao na kuwapa mwongozo.
Kikosi cha Simba SC kimeondoka leo asubuhi kwenda Arusha tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya JKT Oljoro Jumamosi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, lakini Haruna maarufu kama Boban na Ngassa wamebaki kwa ajili ya kikao hicho.
Habari zimesema, wachezaji hao watapanda ndege baada ya kikao hicho kwenda kuungana na wenzao Arusha kwa ajili ya mchezo huo. 
Kumekuwa na habari kwamba wachezaji hao wamesimamishwa kwa utovu wa nidhamu, lakini ukweli ni kwamba hawajasimamishwa na wala uongozi hauna dhamira ya kufanya hivyo kwa kuwa hawana kosa kubwa, zaidi ya kutofautiana na kocha.
Katika kikao cha leo, uongozi utawatajia wachezaji hao kesi iliyowasilishwa dhidi ya na kocha Liewig na kisha kusikiliza utetezi wao, na baada ya hapo watatafuta suluhu.
BIN ZUBEIRY inafahamu Simba haiko tayari kuvuruga timu yake kwa sasa zaidi ya kujipanga sawasawa, ili kuhakikisha wanajiimarisha kwenye mbio za kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.