MAMLAKA ya udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA) imetoa siku 21 kwa shirika la Umeme Tanzania (TANESCO ) kuwasilisha majibu dhidi ya hoja zilizotolewa na wateja wa shirika hilo jijini Mbeya


MAMLAKA ya udhibiti wa huduma za nishati na maji(EWURA) imetoa siku 21 kwa shirika la Umeme Tanzania (TANESCO ) kuwasilisha majibu dhidi ya hoja zilizotolewa na wateja wa shirika hilo jijini Mbeya kuhusu kubambikiwa deni la zaidi ya Sh.Mil.16 katika nyumba za kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya.
Katika barua yenye kumbukumbu nambari EWURA/33/1/194/2 ya januari,4,2013 iliyoandikwa na Mkurugenzi wa Mkuu wa Eura Tanzania,Haruna Masebu kwenda kwa mkurugenzi mtendaji wa Tanesco Makao makuu imeliagiza shirika hilo kusitisha deni na makato yake kuendelea kuwapatia huduma ya umeme wateja hao hadi mamlaka itakapotoa uamuzi wa shauri hilo.
Barua hiyo yenye kichwa cha habari Taarifa ya Malalamiko na wito wa kuleta maelezo yako dhidi ya malalamiko ya wateja wa Tanesco Mbeya kubambikiwa deni nakala pia imesambazwa kwa Waziri wa nishati na madini,Prof.Sospeter Muhongo (MB),Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mbeya na walalamikaji.
Mkurugenzi Masebu amesema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 5(1) cha kanuni za taratibu za kutatua migogoro za Ewura [The energy and Water Utilities regulatory Authority(Consumer complaints settlement procedure) Rules,GN.No.30/2008},Tanesco inatakiwa kuwasilisha majibu dhidi ya malalamiko yaliyotolewa na wateja wake katika gazeti moja la kila siku(siyo Jambo leo) la Jumatano,Januari,2,2012.
Inahitimisha sehemu ya maagizo ya Mkurugenzi wa Ewura kuwa Tanesco izingatie kuwa kushindwa kuwasilisha utetezi wake ndani ya muda uliotajwa kutaiondolea haki yake ya kusikilizwa na Ewura itaendelea kufanya maamuzi katika shauri hilo kwa kuzingatia hoja za upande mmoja kwa mujibu wa kanuni zilizotajwa na kwamba majibu ya Tanesco kwa ewura walalamikaji wapewe nakala.
Wakizungumzia barua hiyo baadhi ya walalamikaji hao ambao ni wapangaji katika nyumba za Kanisa Katoliki jimbo la Mbeya zilizonunuliwa kutoka shirila la reli Tanzania (TRC) Aidary Khalfan na Mohamed Tamimu wamesema kuwa tangu wamepokea barua hiyo bado Tanesco hawajatekeleza agizo la kuwarejeshea huduma ya umeme na nakala ya barua ya kujibu hoja Ewura ambapo ilipaswa na wao wamapate nakala lakini hawajapelekewa(walalamikaji).
 
Wametoa wito kwa Viongozi wa ngazi za juu wa shirika hilo kuwa makini na baadhi ya watumishi wao wa ngazi za chini kwani wanaweza kulipeleka Shirika kubaya kutokana na kufanyakazi kwa maslahi yao binafsi, kulifanya shirika kama mali yao wakati ni la watanzania na hivyo kuweza kulitia hasara kubwa.
Hata hivyo wamesema licha ya kupata majibu ya kejeli na kukatishwa kabisa tamaa na wafanyakazi wa Tanesco kuhusiana na madai yao hawakukata tamaa na kuamua kufikisha sauti hiyo kupitia vyombo vya habar.
Aidhai wametoa wito kwa watanzania kuvitumia vyombo vya habari pindi wanapoona wananyanyasika ili wahusika waweze kuwasaidia kuliko kukaa kimya na kuendelea kuteseka.
Meneja wa Shirika la Tanesco,Mkoa wa Mbeya enginia ,John Bandiya alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu kukaidi agizo la Ewura,amesema barua ilielekezwa kwa mkubwa wake ambaye Mkurugenzi mtendaji makao makuu hivyo hana lolote la kusema.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI