REBECCA ADLINGTON WA UINGEREZA AJIUZULU KUOGELEA


 Rebecca Adlington akitangaza kujiuzulu mashindano ya kuogelea mbele ya waandishi wa habari.
Rebecca Adlington akiwa katika picha ya pamoja na wazazi wake, muda mfupi kabla ya kutangaza kujiuzulu mashindano ya kuogelea mbele ya waandishi wa habari.
Rebecca Adlington katika akiwa na washindi wengine baada ya kujitwalia medali katika mchezo wa kuogelea.
Rebecca Adlington katika akiwa na washindi wengine baada ya kujitwalia medali katika mchezo wa kuogelea.
Rebecca Adlington akipozi akiwa ameshikilia medali ya dhahabu na bendera ya taifa ya Uingereza.
Rebecca Adlington akionesha tuzo ya OBE aliyotunukiwa na Malkia Elizabeth wa II wa Uingereza.
LONDON, England
'Nalichukia sana neno nastaafu. Napenda sana kuogelea, lakini kufanya hivyo kiushindani kwa sasa sitoendelea, nimefikia tamati. Daima nitendelea kuogelea hata nikiwa na umri wa miaka 90'
BINGWA wa medali mbili za dhahabu za michuano ya Olimpiki katika mchezo wa kuogelea, Rebecca Adlington leo amethibituisha rasmi kustaafu katika katika uogeleaji wa ushindani.
Majaaliwa na ya muogeleaji huyo kijana mwenye umri wa miaka 23 katika mchezo huo yalizua maswali makuu, tangu mkali huyo alipotwaa Shaba mbili za Olimpiki ya majira ya joto mwaka jana jijini hapa.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jana jijini hapa, Rebecca mzaliwa wa Mansfield alithibitisha kuhitimisha zama zake katika mchezo huo, akiwa ametwaa ubingwa wa Olimpiki, dunia, Ulaya na michuano ya Commonwealth.
'Nalichukia sana neno nastaafu. Napenda sana kuogelea, lakini kufanya hivyo kiushindani kwa sasa sitoendelea, nimefikia tamati. Daima nitendelea kuogelea hata nikiwa na umri wa miaka 90.'
Rebecca akaongeza kuwa: 'Kwa hakika siwezi kushinda nao (waogeleaji vijana). Siwezi kushinda tena katika ngazi hiyo, nahitaji kujiweka mbali kidogo wakati huu hali yangu ikitengemaa.
'Ilikuwa muda huo. Beijing ilibadili maisha yangu yote, kila mmoja alitaka kujifunza kuhusu mimi. Ulikuwa wakati bora zaidi katika zama zangu mchezoni. Nina furaha sana kuona rekodi yangu ya dunia ingali imesimama,' alisema Rebecca katika mkutano wake huo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA