SASA WATEJA WA NMB BANK KUWEKA FEDHA KWA KUTUMIA M PESA


NMB leo hii  imeweka historia  kwa kuanzisha huduma mpya itakayowawezesha wateja  wake nchini kuweza  kuweka  amana zao kupitia mawakala zaidi ya 40,000 wa M-Pesa Nchi nzima. Pia wateja wa NMB wataweza kutuma fedha kutoka NMB kwenda MPESA.  NMB na Vodacom zimezindua huduma hiyo rasmi leo hii kwenye makao makuu ya NMB.


Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Mark Wiessing,( kulia) na  Afisa Mkuu wa Biashara- M-Pesa- Jacques Voogt wakitia sahihi katika mkataba kam ishara ya ushikiano na makubaliano ya kumwezesha mteja wa NMB kufanya muamala wowote kwenye akaunti yake kwa kutumia huduma ya M-Pesa wakati maofisa wa NMB na Vodacom wakishuhudia.
Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Mark Wiessing,( kulia) na  Afisa Mkuu wa Biashara- M-Pesa- Jacques Voogt wakibadilishana mkataba kama ishara ya ushikiano na makubaliano ya kumwezesha mteja wa NMB kufanya muamala wowote kwenye akaunti yake kwa kutumia huduma ya M-Pesa wakati maofisa wa NMB wakishuhudia.
Sasa mtu yeyote au wateja wa NMB hawatahitaji kwenda ndani ya benki ili kuweka fedha kwenye akaunti kwani sasa wataweza kuweka fedha kwenye akaunti ya NMB bila kwenda tawini.  Pia sasa wateja zaidi ya 800,000 wa NMB mobile wataweza kutuma fedha kwenda MPESA.

 Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo, Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bw.Mark Wiessing, “alisema “Ni huduma ya aina yake ambayo itawezesha mzunguko wa miamala baina ya wateja na benki kufanyika kwa urahisi na haraka, jambo litakalosaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki sanjari na kuboresha hali ya maisha na uchumi kwa watanzania wote mijini na vijijini”.

 Akizungumza kwa niaba ya Vodacom, Afisa Mkuu wa Biashara- M-Pesa- Jacques Voogt, amesema, "Hii ni hatua nyingine ambayo tunaifikia leo. Kampuni ya Vodacom inaendelea kupanua mtandao wake wa huduma ya M-Pesa kwa kushirikiana na benki ya NMB ambapo kwa kufanya hivyo itaruhusu wateja wa NMB kuweza kuweka amana zao kwenye akaunti zao kwa urahisi zaidi. Wakati huo huo, tunawaleta wateja wa benki ya NMB karibu na akaunti za benki zao kwa kuwezesha pesa kutoka benki kwenda M-Pesa. "

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.