SERIKALI YAFUNGUA GHALA LA KISASA LA KUHIFADHIA DAWA KATIKA MAKAO MAKUU YA BOHARI YA DAWA (MSD), DAR ES SALAAM


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein Mwinyi 
(wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria upokeaji wa
 magari  maalumu ya kusafirishia chanjo kwa 
kuzingatia mnyororo badiri. Kushoto ni Mwakilishi 
Mkazi wa Shirika la kuhudumia watoto duniani 
(UNICEF), DK. Jama Gulaid, Balozi wa Marekani 
nchini Alfonso Lenhardt na Mbunge wa Temeke 
Abbas Mtemvu. Mbali na kupokea magari hayo 
kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, Dk. Mwinyi 
alifungua Jengo la Kisasa la ghala la 
kuhifadhi 
dawa katika Makao Makuu ya Bohari ya dawa 
Dar es Salaam leo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein Mwinyi 
(wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria upokeaji 
wa magari  maalumu ya kusafirishia chanjo kwa
 kuzingatia mnyororo badiri. Kutoka kushoto 
ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), 
Cosmas Mwaifwani,  Mwakilishi Mkazi wa Shirika 
la kuhudumia watoto duniani (UNICEF), 
DK. Jama Gulaid, Balozi wa Marekani nchini 
Alfonso Lenhardt . Mbali na kupokea magari hayo 
kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, Dk. Mwinyi 
alifungua Jengo la Kisasa la ghala la kuhifadhi 
dawa katika Makao Makuu ya Bohari ya dawa 
Dar es Salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), 
Cosmas Mwaifwani (kulia),akimuelekeza jambo 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein 
Mwinyi (kushoto), juu ya ubora wa ghala  jipya la 
kisasa la kuhifadhia dawa, baada ya kulizindua 
katika Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD), 
Dar es Salaam. 
Wa pili kushoto ni Mbunge Viti maalunu Martha 
Mlata na Balozi wa Marekani nchini  
Alfonso Lenhardt. 
(Picha habari na www.mwaibale.blogspot.com)
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein 
Mwinyi, 
akikata utepe kuashiria kupokea madawa na 
vifaa tiba vilivyotolewa na Madaktari wa Afrika 
kwa Serikali. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi 
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas 
Mwaifwani, Mkurugenzi wa Tiba wa 
Madaktari Afrika, 
Dk.Dilan Ellegale na Balozi wa Marekani 
nchini Alfonso Lenhardt.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi 
(wa tatu kushoto waliokaa), akiwa katika picha ya 
pamoja na wafanyakazi wa Bohari ya madawa 
(waliosimama nyuma). Kutoka kushoto ni Kaimu 
Mganga Mkuu wa Serikali Donan Mmbando, Balozi 
wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt, Kaimu 
Mkurugenzi  Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), 
Cosmas Mwaifwani, Mbunge wa Kigamboni 
Dk. Faustine Ndungululile, Mwakilishi Mkazi 
wa Shirika la kuhudumia watoto duniani 
(UNICEF), 
DK. Jama Gulaid na Mbunge wa Temeke, 
Abbas Mtemvu.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein 
Mwinyi (wa tatu kushoto waliokaa), akiwa 
katika picha ya pamoja na wawakilishi wa 
Shirika la Afya Duniani ( (waliosimama nyuma). 
Kutoka kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa 
Serikali Donan Mmbando, Balozi wa Marekani 
nchini Alfonso Lenhardt, Kaimu Mkurugenzi  

Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas 
Mwaifwani, 
Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine 
Ndungululile,  
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la 
kuhudumia 
watoto duniani (UNICEF), 
DK. Jama Gulaid na 
Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi 
(wa tatu kushoto waliokaa), akiwa katika picha ya 
pamoja na wajumbe wa Kamati ya Afya ya Bunge 
(waliosimama nyuma). Kutoka kushoto ni Kaimu 
Mganga Mkuu wa Serikali Donan Mmbando, 
Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt, 
Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Bohari ya Dawa 
(MSD), Cosmas Mwaifwani, Mbunge wa 
Kigamboni 
Dk. Faustine Ndungululile, Mwakilishi 
Mkazi wa Shirika la kuhudumia watoto duniani 
(UNICEF), DK. Jama Gulaid
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein 
Mwinyi (hayupo pichani) akiwaongoza wageni 
waalikwa wakati akipokea magari mawili
 maalumu ya kusafirishia dawa.
Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Bohari ya Dawa 
(MSD), Cosmas Mwaifwani (kulia), akiwaongoza 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein 
Mwinyi na Balozi wa Marekani nchini  
Alfonso Lenhardt, 
kwenda kuzindua magari maalumu ya 
kusafirishia dawa.
Mfanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), akionesha 
jinsi 
ya kubeba dawa ndani ya bohari hiyo kwa 
kutumia toroli maalumu.
Dereva wa Bohari ya Dawa (MSD), akionesha 
jinsi 
ya kubeba dawa ndani ya bohari hiyo kwa 
kutumia foku lifti.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein 
Mwinyi (katikati), akiwa na viongozi mbalimbali 
kwenye hafla hiyo
Wafanyakazi wa Bohari ya Madawa (MSD), wakiwa 
kwenye hafla hiyo

Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dk.Donan 
Mmbando 
akihutubia kwenye sherehe hiyo.

Na Dotto Mwaibale

RAIS Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara ya Afya na 

Ustawi wa Jamii na Jeshi la Polisi

nchini kufanya msako na kuwafichua watu wote 

watakaopatikana na dawa za Serikali

katika maduka binafsi.

Maagizo hayo ylitolewa na Waziri wa Afya na 

Ustawi wa Jamii kwa niaba ya Rais Kikwete

ambaye angekuwa mgeni rasmi kwenye 

sherehe za 
ufunguzi wa ghala la kisasa la

kuhifadhia dawa katika Makao Makuu ya Bohari ya

 Dawa jijini Dar es Salaam leo.

"Natambua kuwa lipo tatizo la dawa na vifaa tiba vya serikali kupatikana katika maduka

ya dawa ya watu binafsi jambo ambalo linanikera sana nawaagizeni wachukukieni hatua

za kisheria wale wote watakao patikana na dawa hizo" 

alisema Rais Kikwete.

Alisema Serikali haiwezi kuendelea kununua dawa 

kwa dharama kubwa na zikaishia

katika mifuko ya watu wachache badala ya wananchi 

walio wengi hususani wa vijijini.

Alisema Bohari ya dawa iliundwa mwaka 1994, 

ikiwa nadira ya kufikisha dawa na vifaa

tiba karibu na wananchi ambapo tumeambiwa 

kuwa 
shughuli za MSD zimepanuka sana

hususani uwezo wa maghala umefikia mita za 

mraba 51,800 na nusu ya hizo ni za

kukodisha kwa watu binafsi.

"Natambua kuwa gharama za ukodishaji wa magahala ni kubwa sana na ni vema MSD

ikawa na maeneo yake yenyewe bila kutegemea 

maghala binafsi" alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete alizielekeza Halmashauri husika katika 

kanda za MSD kuisaidia Bohari ya

dawa kupata maeneo mkakati ya uhifadhi wa dawa 

na maeneo waliyonayo tayari

yaweze kupewa haki miliki.

Alisema chanjo ni hatua muhimu kwa ajili ya ya afya 

za mama na mtoto ambapo mpango

wa taifa wa chanjo ulianza mwaka 1975 ukiwa unatoa 

chanjo dhidi ya magonjwa kama

KifuaKikuu, Polia, Surua, Dondakoo, kifaduro na

 Pepo Punda.

Alisema magonjwa mengine yaliyongezeka ni kinga 

dhidi ya Homa ya Ini, Homa ua Uti

wa mgongo, nimonia na kinga dhidi ya magonjwa 

ya kuhara.

Rais Kikwete aliongeza kuwa kinga ni haki ya kila 

mtoto hivyo mahitaji ya chanajo

yamekuwa yanaongezeka kwaka hadi mwaka 

kutokana na ongezeko la idadi ya watu.

"Ongezeko la idadi ya chanjo pamoja na ongezeko 

la aina za chanjo imesababisha kuwa

na hitaji kubwa la maeneo ya kuhifadhi chanjo na kuzisambaza" alisema Kikwete.

Alisema Utunzaji wa chanjo unahitaji mfumo wa 

mnyororo baridi hivyo kuhitaji vyumba

maalumu vyenye ubaridi, pamoja na gari lenye 

vifaa vya kutunza ubaridi huo ili

kuhakikisha mnyororo baridi.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein 

Mwinyi alisema ufunguzi wa gahala hilo

ni sehemu ya kutekeleza mpango mkakati wa MSD wa 

kuhakikisha upatikanaji wa dawa

na vifaa tiba vyenye ubora unaokubalika na kwa 

bei nafuu.

"Mpango huu umeandaliwa kwa kuzingatia Sera ya Afya ya kufikisha huduma bora za

afya kwa kila Mtanzania" alisema Mwinyi.

Alisema vyumba vya kuhifadhia chanjo na magari 

maalumu ya kusafirishia chanjo

uliozinduliwa vitasaidia katika kutunza na 

kusafirisha chanjo katika hali ya ubaridi kwa

mujibu wa miongozo ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ambayo Tanzania

inatekeleza.

Alisema ghala hilo linauwezo wa kuhifadhi 

dawa na 
vifaa tiba lina mita za mraba 4,280

na kuwa limejengwa kwa msaada wa Serikali ya 

Marekani na Mfuko wa Dunia wa

Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na

 limegharimu jumla ya Dola za Marekani

milioni 4 sawa na takribani sh.bilioni 6.4 za Kitanzania.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), 

Cosmas Mwaifwani alisema ujenzi

wa ghala hilo ni matunda yaliyotokana na 

safari za 
Rais Kikwete nje ya nchi hususan

Marekani ambapo mei 2 mwaka 2009 akiwa katika

 ziara nchini Marekani Rais wa nchi

hiyo Barack Obama aliahidi kuendelea kutoa 

misaada katika maeneo mbalimbali

likiwemo la kuboresha huduma za kupambana na 

maradhi ya Ukimwi kupitia shirika la

PEPFAR.

Alisema moja ya miradi inayoratibiwa na PEPFAR 

ni ujenzi wa maghala makubwa katika

kanda za Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Tanga 

na Tabora.

Mwaifwani alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais 

Kikwete kwani matokeo ya juhudi zake

zimeleta matunda ambayo yanaonekana kwa Taifa.

Alisema ukamilishwaji wa miradi hiyo utaisaidia 

Bohari ya Dawa kukomboa jumla ya

shilingi za Tanzania bilioni 1 katika mwaka 

ujao wa 
fedha ambazo wamekuwa wakilipa

kwa ajili ya kukodi maghala ya watu binafsi kwa ajili 

ya kuhifadhi dawa, vifaa tiba na

vitendanishi kabla ya kusambazwa kwa walengwa.

Alisema Bohari ya Dawa imeendelea kutekeleza jukumu lake la msingi la kusambaza

dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya hapa nchini 

kwa niaba ya Serikali.

Aliongeza kuwa katika kutekeleza majukumu hayo 

Bohari ya Dawa imefanikiwa

kufanikisha upatikanaji wa dawa ambapo imefikia 

kati ya asilimia 70 hadi 75 ya mahitaji

dhidi ya asilimia 44 wakati Taasisi hiyo ilipo 

anzishwa mwaka 1994.

Alisema mikoa 10 imeingizwa katika mfumo wa 

kufikisha dawa moja kwa moja hadi

vituo vya afya na mikakati imewekwa ya kuingiza 

mikoa yote ya Tanzania katika mfumo

huo kuanzia julai 2013 na kuwa mkakati huu 

unazihusu pia hospitali za Wilaya, Mikoa na

Hospitali za Rufaa.

Mwaifwani alisema MSD imefungua mfumo 

mpya 
wa kisasa wa TEHAMA (EPICOR) ili

kurahisisha shughuli za usambaji ambao pia 

umefadhiliwa na USAID.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.