SIMBA YAMUANDALIA MAPOKEZI MAZITO MALKIA WA NYUKI

Rahma Al Kharoos

Na Princess Asia
KLABU ya Simba SC imemuandalia mapokezi ‘baab kubwa’ mfadhili wao wa ziara ya Oman, Mama Rahma Al Kharoos, Malkia wa Nyuki, anayetarajiwa kutua nchini Jumanne.
Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga ameiambia BIN ZUBEIRY leo mchana kwamba, wanachama na wapenzi wa klabu hiyo wanatakiwa kufika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam siku hiyo kumpokea mfadhili huyo.
“Mama huyu ametusaidia sana kwa kweli, katika kambi yetu ya Oman alitumia zaidi ya Sh. Milioni 80 ambazo ziliisaidia sana timu kwa maandalizi, kwa hiyo tunaomba twende tukampokee siku hiyo, ili kulipa fadhila kwake,”alisema Kamwaga.
Kamwaga alisema kwamba Mama Rahma atakuwa Mkuu wa Msafara wa Simba itakapokwenda nchini Angola kucheza na Libolo ya huko katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu wiki iliyopita, Simba iliweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na hatua hiyo kwa ufadhili kamili wa Malkia wa Nyuki. Hayo yalikuwa majibu kwa wapinzani wao wa jadi, Yanga SC walioweka kambi ya wiki mbili pia nchini Uturuki.
Matunda ya ziara ya Oman ni Simba kuanza Ligi Kuu ya kishindo ikiitandika 3-1 African Lyon na keshokutwa itaingia kwenye mchezo wa pili kusaka pointi dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI