0 Comments

NIMR MWANZA YAHUSISHWA NA FREEMANSON, YAKANA NA KUSEMA NI UVUMI TU

DAILY NKOROMO, MWANZA
TAASISI ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) mkoani Mwanza imekanusha kujiunga au kuwa na uhusiano wowote na kundi la Freemanson.

Imesema, uvumi ulioenezwa katika baadhi ya maeneo ya jiji la Mwanza na mikoa jirani ya Geita na Shinyanga kuwa imejiunga na Freemanson, umesababisha kupuangua wanachama wake kwa asilimia kumi.

Akizungumza jijini Mwanza, Mkurugnezi wa NIMR Mwanza, John Chagula alisema wilaya ambazo utendaji wake unakwamishwa na uvumi huo ni pamoja na Magu na Kwimba mkoani Mwanza, Kahama (Shinyanga) na Geita.

“Uvumi kwamba NIMR tunashirikaiana na Freemanson, ambao siyo kweli imeathili na kushusha utendaji wetu wa kazi kwa asilimia kumi, kabla ya kutokea wanachama wetu walikuwa asilimia 90 sasa wameshuka hadi asilimia 80 katika maeneo hayo.” alisema.

Alifafanua kwamba, hata baadhi ya wanachama wake waliobaki wameingiwa na hofu na kuwafanya wasishirikiane na taasisi hiyo kikamilifu na hivyo kuwaomba wananchi wapuuze uongo huo ili waendelee kufanyiwa uchunguzi na kupunguza magonjwa.

“Tunawaasa wananchi waondoe dhana ya Freemanson katika mawazo yao , hatuhusiani nayo kabisa na hatujui chochote kuhusu freemanson.” Alieleza Chagula

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA