TAMKO LA WALIOKUWA VIONGOZI WA CHADEMA - MBEYA, KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA KUHUSU KUHAMIA NCCR-MAGEUZI TAREHE: 03/02/2013.

Moses Aliko Mwasubili (bulldozer)

Sarah A. Mwaseba


Ndugu wanahabari, salaam!
Ndugu wanahabari, Kwanza hatunabudi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ulinzi anaotupatia na uwezo wa kutambua fikra zetu. Tunawashukuru viongozi wetu wa NCCR - Mageuzi kwa kututambua na kufika Mbeya ili kutupokea. 
Pia tunawashukuru waandishi wa habari wote kwa kazi nzito inayowafanya muwe maadui na marafiki katika utekelezaji wa majukumu yenu kwa Taifa letu. Mungu na awajalie ulinzi mkuu katika kutekeleza majukumu yenu.   
Ndugu Wanahabari,  
Sisi ni sehemu tu tunaohamia NCCR-Mageuzi kutoka CHADEMA na vyama vingine. Kimsingi tumetangulia na tumeamua kujitokeza mbele ya watanzani kupitia kwenu wanahabari ili kuwa mashuhuda wa kisiasa
Wapo wenzetu wanaohama kimya kimya kimwili na kifikra. Lakini wapo wengine tuliowaacha huko kwenye matawi yetu tunakwenda kuwapokea na kuanza nao kazi mpya katika Demokrasia ya kweli na mfumo bora wa kiutawala ndani ya NCCR Mageuzi.
Wapendwa wanahabari, harakati zetu zina historia tofauti katika siasa za nchi hii. Wapo ambao leo hii wanarudi NCCR baada ya kuhama miaka kadhaa iliyopita. 
Lakini wapo pia wanaotoka  CCM na CUF. Lengo letu ni kuitoa CCM madarakani na kujenga utawala wa sheria na Demokrasia ya kweli ndani ya vyama vyetu. 
Kwa furaha kubwa kabisa tunapenda kuchukua fursa hii kuwatangazia wana Mbeya na umma wa Watanzania kwa kuvunja ukimya na sasa  tunatangza rasmi kujiunga na Chama Cha NCCR- Mageuzi ( National Convention For Construction and Reform- Mageuzi) na tunasema tena kuwa, tumejiunga kwa hiari yetu kutokana na kuikimbia CHADEMA kwa mambo yake ambayo kwa uchache tunayaeleza kama ifuatavyo:
·         Uongozi wa kitaifa umefeli kujenga demokrasia ya kweli ndani ya chama kwa kukumbatia ufisadi wa kutumia vibaya ruzuku ya chama. 
Chadema mikoani imebaki ni kujichangisha fedha kwa kila tukio la ujenzi wa chama utadhani hakuna pesa za ruzuku na michango ya wafadhili.
·         Uongozi mbovu wa Mhe; Mbowe na dk. Slaa kwa kushindwa kusimamia katiba ya chama katika kutatua migogoro ya chama na kuishia kuwa na mbinu ya kufukuza wanachama wema kwa majungu wanayoyajenga wenyewe. 
·         A  tukisema ukweli wa ouvu wao jamii haiwezi kuamini. Wanajidanganya!!!!  Hii ni ishara ya kufinyanga katiba na kutoiheshimu dhana ya nguvu ya umma.
·         Chama kujaa utashi wa nguvu ya umma na kulazimisha maandamano, migomo kwa vitu visivyo na ulazima.
 Sisi hatuwezi kuamini pamoja na watu walio na malengo ya kuleta fujo kitaifa kwa kisingizio cha kutafuta ukombozi mpya wa taifa. 
·         Hatua ya kuwafukuza fukuza viongozi bila kuwasilikiliza hususani wa nyanda za juu kusini.
·         Dk. Slaa kulipwa mamilioni ya pesa kama mshahara wake na posho lukuki amejikusanyia na watu anaowataka Makao Mkuu. 
·         Akina mama Mbeya walihamasishwa kuwa tuwe tunampokea mchumba wa Katibu mkuu slaa kama mke wa raisi kumbe ni mwanachama wa kawaida anayetumia vibaya rasilimali za chama.
·         Uwezo mdogo wa kutekeleza ahadi alizoahidi mbunge wa mjini ‘joseph mbilinyi’ kwa wananchi wa mbeya. Ameacha kuufanya ubunge kuwa ni taasisi nyeti ya umma na ameamua kuutumia kama jukwaa la muziki na ameonesha Mbeya hatuna uwezo wa maendeleo ya pamoja.  
 Wakati wa kampeni aliahidi kujenga mabwawa ya samaki, bandari ya nchi kavu, vifaa vya hospitalini, benki ya wana Mbeya, umoja wa akina mama, vikundi vya ujasiliamali vya kijamii, kuinua wasanii wa mbeya, kulifanya jiji la mbeya liwe mfano wa kuigwa Tanzania. 
Pia aliahidi kutatua kero ya elimu (shule za kata), usafi wa jiji, mpango mzuri wa masoko ndani ya jiji. Lakini hadi leo hakuna anachofanya zaidi na hata bungeni na kupandikiza chuki za kukataa kupokea Raisi wa nchi anapokuwa na ziara mkoa wa mbeya. 
·         Mbunge ameendelea kuchochea wanachama asiowataka wafukuzwe nafasi za uongozi na anaowataka walindwe. 
Aliwahi mwambia DK, Slaa kuwa akimtoa mwenyekiti wa wilaya ya mbeya mjini basi, yeye anarudisha kadi; masikini bila kujua mzee wa watu dk. Slaa akamsikiliza na akageuka mbogo kwenye kikao cha ndani na kuamua kuwalinda waharifu wa siasa za Mbeya na kuwafukuza ambao ‘SUGU’ hawataki.  Dk. Slaa alionesha uwezo mdogo wa kudadavua mambo ya maneno ya majungu. 
Tumechukua uamuzi huu mzito wa kuhama chadema na kujiunga na NCCR-Mageuzi kwa kuwa NCCR kwa matendo kimeonekana kuwa chama cha UTU na chenye misingi bora ya usawa, uheshimu wa haki za wanachama na watanzania na chenye mshikamano wa kweli.
S/N
JINA MWANACHAMA
WADHIFA NDANI YA CDM
KATA/TAWI
1:
Moses Aliko Mwasubili (bulldozer)
Katibu mwenezi wa wilaya
Mbeya mjini
2:
Emmanuel Amani Mwangoka (Cash Money)
Mpambe wa mbunge/mwanachama
Mbeya mjini
3:
Magrethy John M ota
Mjumbe wa kamati tendaji
Kata ya Isyesye
4:
Hosea A. Mwangoje
Mjumbe kamati tendaji na MC Kampeni za mbunge – SUGU
Mbeya mjini
5:
Sarah A. Mwaseba
Mwenyekiti wa BAWACHA
Kata ya Isyesye
6:
Emmanuel Nehemiah Ngogo
Mwenyekiti
Tawi la Tawi
7:
William Swila
Katibu mstaafu wa Wazee
Mkoa wa mbeya
8:
Jonathani Mwakalinga
Katibu mwenezi  wa Kata
Kalobe
 Kimepitia migogoro mingi na ya kutisha lakini bado ni imara na hivyo ni vema watanzania wakajenga imani na chama Komavu kuliko CHADEMA ya watu wachache na iliyo furika majungu na ukabila pia haina ukomavu na uzoefu wa migogoro. Migogoro kidogo tu iliyopo wamepoteana na bado wameandaa migogoro mingi ya uchaguzi wa ndani ya chama.
Imetolewa na sisi:  
Majina ya wanaohama toka CHADEMA kuingia NCCR - MAGEUZI.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA