Tume ya Mabadiliko ya Katiba yakutana na Wawakilishi wa Makundi ya Watu wenye Ulemavu
Mwenyekiti
wa kamati ya uwasilishaji wa mapendekezo ya muundo wa mabaraza ya
Katiba kwa jamii ya watu wenye ulemavu, Bw. David Nyendo (kushoto)
akiwasilisha maoni yake ya kamati hiyo kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
katika mkutano baina yao uliofanyika leo (jumatano Feb. 13, 2013) katika
ofisi za makao makuu ya Tume Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mjumbe wa
Tume, Dkt. Salim Ahmed Salim.
Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia)
akizungumza na wawakilishi wa makundi ya jamii ya watu wenye ulemavu
ukiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw. David Nyendo (kushoto) mara
baada ya kufika katika makao makuu ya Tume leo (jumatano Feb. 13, 2013)
kuwasilisha mapendekezo yao juu ya muundo wa mabaraza ya Katiba kwa
jamii ya watu wenye ulemavu. Wa pili kushoto ni Mjumbe wa Tume, Dkt.
Salim Ahmed Salim.
Mkalimani
wa lugha za alama kwa watu wenye ulemavu wa kusikia kutoka Umoja wa
Miradi ya Viziwi Tanzania (UMVITA), Bi. Ruth Hope akisaidia uelewa wa
lugha ya mawasiliano kwa watu wa jamii ya walemavu wa kusikia katika
mkutano baina yao na Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Walemavu hao waliunda
kamati iliyokutana na Tume ili kuwasilisha mapendekezo yao juu ya
muundo wa mabaraza ya Katiba kwa jamii yao.(PICHA NA TUME YA KATIBA)
Comments