Wafanyakazi wa AIRTEL Tanzania wawapiga 'jeki' Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum Shule ya Msingi Msasani

Afisa Rasilimali Watu wa Airtel Tanzania, Bi. Doris Kibasa (kushoto), akikabidhi vitabu kwa Mwalimu Mkuu wa Kitengo cha watoto wenye mahitaji maalumu wa Shule ya Msingi ya Msasani, Lessy Nyambo, mchango uliotolewa na wafanyakazi wa Airtel Tanzania kwa watoto wa shule hiyoiliyopo jijini Dar es Salaam jana.
Watoto wenye mahitaji maalumu wa Shule ya Msingi ya Msasani wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel Tanzania, baada ya kupokea msaada wa vitabu kwa walimu na wanafunzi wa shule hiyo vilivyotolewa kwa ushirikiano wa wafanyakazi hao, ili kusaidia ufundishaji wa masomo ya elimu  kwa watoto wa mahitaji maalumu.

******************************************
   . Yatoa vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya million 3/-  

    . Yapunguza uhitaji wa vitabu hadi uwiano wa 1:1

Dar es salaam 2013: Katika kuchangia shughuli za kijamii, wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkoni Airtel kwa pamoja wameshiriki katika kuchanga na kusaidia wanafunzi wa shule ya watoto wenye mahitaji maalumu iliyopo Msasani jijini  Dar es Salaam.

Wafanyakazi hao wamekusanya kiasi cha shilingi milioni 3 zilizotumika kununua vifaa mbali mbali vya kufundishia.

Akizungumzia mpango huo maalum wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo  Afisa Rasilimali watu wa Airtel Tanzania, Bi. Doris Kibasa alisema  kuwa mkakati huo umewahusisha wafanyakazi wa Airtel katika vitengo tofauti na kuwashukuru kwa kujipanga wao wenyewe na kutumia muda wao kwa kuwakumbuka watoto hawa kwa namna hiyo.

Zoezi hili limewezesha upatikanaji wa jumla ya vitabu vyenye thamani shilingi milion 3 kwa shule ya msasani na kupunguza uhaba wa vitabu kutoka kitabu kimoja kwa watoto watatu hadi kitabu kimoja kwa kila mtoto mmoja.

“Tumeona mahitaji ya wanafunzi hawa tulipotembelea shule hii mwishoni mwa mwaka  jana. Na kuamua kujipanga ili kuweza kuwasaidi wadogo wetu na majirani zetu ili waweze kufika hapa tulipo sisi leo. Tunaamini kwa kufanya hivi tutakuwa tumeweza kuinua maisha ya watoto hawa na kiwango cha Elimu hapa Tanzania” alisisitiza Bi. Kibasa.

nae Mwalimu Mkuu wa kitengo cha watoto wenye mahitaji maalum Bw, Lessy Nyambo alisema msaada huo ni mkombozi kwa wanafunzi hao kwani utawawezesha wanafunzi hao kuwa na kitabu kimoja kimoja badala yakutumia kitabu kimoja wanafunzi wawili mpaka watatu.

 Amesema kwamba wanafunzi hao wanakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi vitakavyowawezesha kuendelea na masomo bila tatizo lolote na hivyo amewahasa mashirika ya umma  na wadau mbalimbali kushirikiana na Serikali katika kusaidia shule za watoto wenye mahitaji maalumu.

Naye mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Msasani, Fatuma Ally aliishukuru Airtel kwa kuweza kuwapatia Vitabu ambavyo vitaweza  kuwasaidia katika masomo yako.

Airtel chini ya mpango wake wa shule yetu imedhamiria kuendelea kuboresh kiwango cha elimu nchi na kuleta mabadiliko katika masomo ya sayansi ili kupata wataalamu wengi wasayansi nchini.

Wiki mbili zilizopita tumetoa msaada wa Vitabu na sare za shule katika shule ya msingi ya Kiromo iliyopo mjini Bagamoyo vyenye dhamani ya shilingi milioni 50 , huku ikitoa msaada wa vitabu kwa shule 4 za sekondari kwa kila mkoa ikiwemo mikoa ya Kagera na Mwanza Lengo ni kufikia shule nyingi zaidi nchi nzima.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*