WANAFUNZI WALIOSHINDA SHINDANO LA INSHA WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

 Afisa Elimu mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mapunda (kushoto) akimkabidhi hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee zawadi ya redio (music sytem) Winfrida Leonard  kutoka shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA – Nakayama iliyopo Rufiji mkoani Pwani ambaye alishika nafasi ya tatu katika mashindano ya kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania. Mashindano hayo yaliandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) ambapo jumla ya wanafunzi 32 kutoka shule nane  walishiriki.
 Faiza Ussi  kutoka shule ya Sekondari ya Sunni Madressa ya mjini Zanzibar alifurahia zawadi ya laptop aliyopewa hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania. Mashindano hayo yaliandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA) ambapo jumla ya wanafunzi 32 kutoka shule nane  walishiriki.
 Washindi kumi walioshiriki  shindano la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA)  wakiwa katika picha ya pamoja hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee na baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.  Wanafunzi 32 kutoka shule nane  walishiriki katika mashindano hayo yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza ambapo mshindi wa kwanza alipata laptop yenye thamani ya dola 600 za kimarekani.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakiwa katika picha ya pamoja hivi karibuni na wanafunzi wanne kutoka shule ya Sekondari ya wasichana ya WAMA-Nakayama walioshiriki    shindano la kuandika insha kuhusu maadili na madhara yake kwa vijana wa Tanzania lililoandaliwa na umoja wa wanafunzi wa Tanzania waliosomeshwa kwa ufadhili wa Japan (JATA)  nakushika nafasi ya tatu, sita, saba na tisa.  Wanafunzi 32 kutoka shule nane  walishiriki katika mashindano hayo yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza ambapo shule ya WAMA-Nakayama aliibuka mshindi wa jumla.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA