WATANO WAUAWA KWA RADI MBEYA




WATU watano wamefariki dunia mkoani Mbeya kwa kupigwa radi katika matukio matatu tofauti likiwemo lililoua ndugu watatu wa familia moja. Wanandugu hao watatu wakazi wa kata ya Nyimbili wilayani Mbozi wamefikwa na mauti Februari 5 mwaka huu majira ya saa saba mchana wakati mvua kubwa iliyoambatana na radi za mara kwa mara ikiendelea kunyesha wakiwa nyumbani. 

Afisa mtendaji wa kata ya Nyimbili Lingtone Nzowa amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Jerumana Halinga(35),David Halinga(5) na Kumi Halinga(3) ambapo pia radi hiyo imemjeruhi mtoto wa miezi tisa ambaye jina lake halikufahamika mara moja. Tukio la pili limetokea katika kijiji cha Magurula kata ya Utengule Usangu Wilayani Mbarali ambapo radi iliyotokana na mvua kubwa imempiga Kasim Sagutangu na kusababisha kifo chake ambapo diwani wa kata hiyo Juntwa Mwalyaje amesema mvua hiyo imenyesha Februari 3 majira ya saa nane za mchana. Tukio la tatu limetokea februari 3 katika kijiji cha Mbagala Kata ya Ilembo wilayani Mbeya ambapo mwanamke Kotanida Petro amefariki dunia baada ya kupigwa na radi akiwa shambani kwake. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa matukio hayo ya vifo vya watu watano vilivyotokana na radi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI