ZIARA YA EBSS YAPAGAWISHA KINOMA DODOMA

Walter Chilambo akipagawisha 


Shabiki wa kike akijiachia kwa Wababa 
Na Princess Asia
WASANII wa Muziki wa Kizazi Kipya walioshiriki shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search, Norman, Husna, Menina, Wababa, Geofrey na Walter jana walionyesha wao ni moto wa kuotea mbali baada ya kuwapagawisha mashabiki zaidi ya elfu tatu waliohudhuria katika ukumbi wa Club Maisha Dodoma.
Show hiyo kali ilianza majira ya saa tano usiku, kwa mkali kutoka THT Ali Nipishe anayetamba na kibao chake cha ‘MY’, na baadaye kumtambulisha Norman Severino ambaye kwa mara ya kwanza alizindua wimbo wake wa ‘Si Wewe’.
Steji ilizidi kuwaka moto pale kijana tokea Dodoma, Godfrey Levis alipopanda kuimba wimbo wake wa ‘MAYA’ na kufuatiwa na malkia kutoka THT, Linah, aliyeimba nyimbo zake zote kali.
Lakini alikuwa ni mwanadada, Nsami aliyeonyesha kwamba wanawake waliopo kwenye tasnia wajipange alipopanda kuimba wimbo wa ‘MUONGO’ na hatimaye mdada wa taarab, Husna akawamaliza wanadodoma kwa kuimba wimbo wake wa ‘Nawamimina’, huku akisifiwa na wengi kwa uwezo wake mkubwa wa kulimiliki jukwaa.
Kama hiyo haitoshi, mashabiki pia waliburudishwa vya kutosha na mwimbaji bora wa kiume wa mwaka, Barnaba, ambaye aliiimba nyimbo zake kama Magubegube na Sorry, ambao unafanya vizuri sana sasa hivi na kuwafanya mashabiki kupiga kelele kwa kumshangilia.
Ukumbi ulizidi kulipuka kwa mayowe baada ya Barnaba kumtambulisha mwanadada mwingine, Menina, ambaye wimbo wake wa Dream tonight unafanya vizuri kwenye vyomba vya habari hapa nchini. Menina, ambaye alimsaidia Barnaba kuitikia wimbo wake wa Wrong Number, alionyesha uwezo mkubwa katika kumiliki jukwaa.
Hadi wakati mshindi wa tatu wa shindano la EBSS, Wababa Mtuka anapanda jukwaani kuimba kibao chake cha ‘My Wife’ watu wa Dodoma walikuwa bado wakishangilia namna alivoonyesha uwezo katika kuimba.
Wa mwisho kabla ya mshindi wa milioni hamsini kupanda alikuwa ni Ben Paul, ambaye aliwakonga nyoyo mashabiki wake kwa nyimbo zake kali kama Pete na Samboira kabla ya kumkaribisha jukwaani Walter.
Mashabiki hao waliokuwa wakimsubiri kwa hamu, walianza kupiga kelele Walter Walter, kabla ya kuwatuliza kwa kuimba wimbo wake mpya wa ‘Siachi’ akifuatiwa wimbo wake mwingine wa ‘Mamy Love’ ambao aliutoa kama zawadi kwa mashabiki zake wa Dodoma.
Walter alipata wakati mgumu jukwaani ambapo mashabiki walimuomba azirudie nyimbo zake zaidi ya mara tatu hali iliyoonyesha kukubalika kwa hali ya juu.
Mashabiki wengi wakizungumza baada ya burudani hiyo walionyesha kuwakubali vilivyo wasanii wa EBSS, huku wakiwatabiria makubwa.
‘Hakika vijana wana vipaji na wanajua hasa kutoa burudani, wakipewa sapoti watafika mbali sana’ alisema Maliki Abdul mkazi wa Dodoma aliyehudhuria burudani hiyo.
Ziara hiyo ya washindi wa Epiq BSS inaelekea Dar mwisho wa mwezi huu kabla ya kuelekea Mtwara.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.