CHELSEA YAICHAPA FC BASEL 2-1, YANUSA FAINALI EUROPA LEAGUE


 David Luiz wa Chelsea akishangilia na wenzake bao lililowapa ushindi wa 2-1 dhidi ya FC Basel ya Uswisi katika katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Kombe la Europa League kwenye Uwanja wa St Jaco-Park jana usiku.
 Luiz akishangilia bao hilo.
 Nyota wa Basel Marco Streller akisikitika baada ya kupoteza nafasi muhimu kuifungia timu yake bao dhidi ya Chelsea.
 Fabian Schar wa Basel akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati
 Fabian Schar akipiga penati hiyo.
Beki wa Basel akilala kumzuia Eden Hazard wa Chelsea, huku Fernando Torres akiwa tayari kutoa msaada.
 Kocha wa Chelsea Rafa Benitez akimpa mpira wa kurusaha nyota wake Victor Moses ambaye alifunga bao la kwanza la Blues kunako dakika ya 12.
  Picha mbili za juu na chini zinamuonesha Moses akishangilia kwa kuruka sarakasi baada ya kuifungia Chelsea bao la kuongoza.
 Moses (13) akiuangalia mpira wake wa kichwa ukitinga nyavuni kuiandikikia Chelsea bao la kwanza.
 Beki wa Basel (14) akimchezea rafu yoso Cesar Azpilicueta wa Chelsea, rafu ambayo ilionekana wazi kuwa ni penati, ingawa mwamuzi hakutoa maamuzi hayo na kuzua malalamiko kwa Benitez.
 David Luiz akimkanyaga nyota wa Basel Phillip Degen. Ingawa refa hakuiona rafuu ipasavyo, kuna kila dalili Luiz akafungiwa mechi moja na Kamati husika itakayomlazimu akose mechi ya marudiano.  
David Luiz akipiga adhabu ndogo 'free kick' iliyozaa bao la ushindi la Chelsea.
BASEL, Uswisi
Katika nusu fainali nyingine, Fernabahce ya Uturuki ikiwa nyumbani Sukru Saracoglu, iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Benfica ya Ureno, ambapo washindi wa mechi hizo wataumana fainali huko Amsterdam Arena, Mei 15
CHELSEA wamenusa fainali ya michuano ya pili kwa ukubwa ngazi ya klabu barani Ulaya ‘Europa League’ baada ya jana usiku kuichapa FC Basel ya hapa kwa mabao 2-1 na kujiwekea mazingira mazuri kuelekea mechi ya mrudiano.
Ikicheza ugenini katika dimba la St Jacob-Park juzi usiku, Chelsea ilitangulia kufunga mapema dakika ya 12 ya mpambano huo, shukrani kwa bao la Mnigeria Victor Moses.
Ni bao lililoonekana kutaka kuitoa dimbani na ushindi, kabla ya Fabian Schar kufunga kwa penati tatatishi dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho kuisawazishia Basel iliyokuwa ikishangiliwa mno na mashabiki wake.
Wakati kila mmoja akiamini pambano linaisha kwa sare ya bao 1-1, katika dakika za nyongeza David Luiz aliifungia Chelsea bao maridadi la ‘mpira uliokufa’ kuipa ushindi muhimu kuelekea marudiano ya Alhamisi ijayo kwenye dimba la Stamford Bridge.
Kocha wa Chelsea, Rafa Benitez alisema kuwa ‘alishangazwa mno’ na mwamuzi Pavel Kralovec kuinyima timu yake penati, baada ya Valentin Stocker kumchezea rafu yoso Cesar Azpilicueta, na kwamba bao la ‘usiku’ ni malipizi ya dhuluma ya mwamuzi huyo.
Benitez akaenda mbali kwa kuwataka nyota wake kutobweteka na ushindi huo, badala yake wajipange ipasavyo kuwakabili wapinzani wao hao katika mechi ya marudiano Mei 2 wiki ijayo na kujikatia tiketi ya michuano hiyo.
"Tulipaswa kufanya jambo kutoruhusu bao lao, ambalo lilikuwa ni zaidi ya motisha kwao mchezoni.
"Mlinda mlango wao pia angekuwa na uwezo wa kuzuia mpira wetu wa adhabu ndogo ‘free-kick’, lakini mwisho wa siku tulifunga bao ambalo kila mmoja nadhani anajua kwamba lilikuwa la haki."
Katika nusu fainali nyingine, Fernabahce ya Uturuki ikiwa nyumbani Sukru Saracoglu, iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Benfica ya Ureno, ambapo washindi wa mechi hizo wataumana fainali huko Amsterdam Arena, Mei 15.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI