CRDB YAPATA FAIDA YA BILION 81

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati akitoa ripoti ya faida ya mapato katika utendaji kazi wa benki hiyo kwa mwaka 2012 jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi, Ally Laay na Mchambuzi Masuala ya Fedha, Mohammed Warsame. (Picha na Habari Mseto Blog)
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Chales Kimei (katikati) akiwa na Mchambuzi wa masuala ya Fedha, Prof. Mohammed Warsame, Mjumbe wa Bodi, Ally Laay, Joyce Nyanza na Mkurugenzi Rasirimali Watu, Dorah Ngaliga.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo.

Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Uudumu kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.

DAR ES SALAAM, Tanzania

IMEELEZWA kwamba mfumuko wa bei umechangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa uchumi hali inayosababisha mazingira magumu ya utendaji kazi katika taasisi za kibenki hapa nchini.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakati akitoa ripoti ya faida ya mapato katika utendaji kazi ya mwaka 2012 ambapo alisema kuwa pamoja na kushuka kwa uchumi benki yake imepata faida ya shs.bilioni 81 sawa na asilimia 113 ambayo ni kubwa kuliko miiaka ya nyuma.
Alisema faida hiyo imepanda kwa asilimia kubwa tofauti na mwaka juzi (2011) ambapo walikuwa na faida ya shs. Bilioni 38 na kuongeza kuwa faida ya mapato kibenki imepungua kwasababau ya hali ya uchumi na ongezeko la bei.
Kimei alisema kuwa, hali hiyo pia husababishwa na ushindani wa kibenki ambao umekuwa mkubwa ambapo hadi sasa kuna benki 50 ingawa kabla ya hapo kulikuwepo na benki 27 nchi nzima.
Aidha, benki hiyo kwa mara ya kwanza katika historia  imefanikiwa kufungua tawi nchini Burundi mwishoni mwa mwaka jana ambako  kuna makao Makuu ya benki ya  CRDB pamoja na matawi madogo madogo  na kwamba ndani ya mwezi mmoja walifanikiwa kupata faida ya shs.bilioni 1.2 .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI