MWAKALEBELA AWASHAURI TFF MAMBO YA RUSHWA MICHEZONI!

images 
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es Salaam
Siku moja baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kumtaka mshambuliaji ,Nsa Job Mahinya ,wa Coastal Union kuwasilisha maelezo yake juu ya madai kuwa alipewa rushwa ya sh. milioni mbili ili asiifunge moja ya timu vigogo vya soka nchini, katibu mkuu wa zamani wa shirikisho hilo, Fredrick Mwakalabela, amesema suala hilo limechukuliwa kwa uharaka sana.
Mwakalabela amesema kauli ya kumwambia kuwa, TFF itachukua hatua kali dhidi ya yake iwapo hatawasilisha maelezo yake kuhusiana na suala hilo ingelenga kumtumia nyota huyo kama chanzo cha taarifa zaidi zinazohusu  masuala ya Rushwa michezoni kwani tatizo hilo lipo hususani mwishoni mwa ligi.
“Kuna mambo mengi yalijitokeza miaka ya nyuma, unakumbuaka suala la Ulimboka Mwakingwe na akina Shabaan Kado wakati simba ilikwenda Morogoro, sidhani kama lilichukuliwa hatua sutahiki,na ndio maana mambo haya yanaendelea kujitokeza chini kwa chini”. Alisema Mwakalabela.
Mwakalebela alisema kuwa , kuna watu wachache wanaotia doa soka letu kutokana na mazoea ya kucheza mchezo mchafu na kupanga matokeo katika mechi muhimu.
Katibu huyo mkuu wa zamani wa TFF alisema kuna wakati Fulani wachezaji hucheza chini ya kiwango wakidaiwa kuwa na mapenzi na timu Fulani wakitarajia kusajiliwa, lakini mambo haya hupuuzwa.
Mwakalebela aliongeza kuwa ,wachezaji wanafahamiana nani kachukua rushwa katika mchezo fulani, cha msingi ni kusimama kidete kupiga vita mchezo huu mchafu unaomaliza kiwango cha soka letu.
Katibu huyo wa zamani wa TFF alisema pia waamzi mara kwa mara wanatuhumiwa kupokea hongo ili kuzisaidia timu fulani.
“Sauala la waamuzi pia linatakiwa lichukuliwe kwa uzito wa juu, kuna mambo fulani yanajitokeza katika michezo, hakika yanatia hofu kubwa, ukifuatilia ripoti za waamuzi huwa zinafanana sana, lakini ukishihudia mchezo unaweza  kugundua kuwa kuna uhuni umefanyika”. Aliongeza Mwakalebela.
Mwakalabela alisisitiza kuwa wakati akiwa kiongozi waamuzi na makamisaa wa mechi walikuwa wanaandika ripoti inayofanana hata kama kulikuwa na matatizo,  suluhisho ni kuwepo mwangalizi maalumu wa waamuzi na hali ya mchezo husika ili kama kuna mambo yasiyoeleweka wahusika wachukuliwe hatua zinazostahiki.
Katibu mkuu huyo wa zamani wa TFF alishauri kuwa mambo haya yaangaliwe kwa jicho la tatu, na kama yatapuuzwa timu zinazojihusishwa na uozo huu zitaendelea kuumbuka kimataifa, pia timu ya taifa itakosa wachezaji wazuri.
Taarifa kutoka TFF hapo jana zilieleza kuwa Job alikaririwa Aprili 3 mwaka huu na kituo cha redio cha Clouds FM katika kipindi cha Amplifier kuwa alipewa kiasi hicho cha fedha na kiongozi wa timu husika ili asiifunge katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom, lakini alipokea fedha hizo na kuifunga timu hiyo.
Baadaye kiongozi huyo alikuwa akimtaka arejeshe fedha hizo. Pia TFF imekiandikia kituo hicho cha redio kutaka nakala ya kipindi hicho ili pamoja na maelezo ya mshambuliaji huyo vipelekwe katika Kamati ya Nidhamu kwa ajili ya hatua za kinidhamu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA