HIZO BURUDANI ZA BONANZA LA TASWA KESHO...WE ACHA TU!

Mkurugenzi wa bendi ya muziki wa dansi ya Extra Bongo, Ally Choky akiimba kuwaonjesha vionjo Waandishi wa Habari leo mchana kwenye ukumbi wa City Sports Lounge, kabla ya Bonanza la Media Day keshokutwa viwanja vya TCC. Wengine kulia ni Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu wadhamini wa tamasha na Super Nyamwela, mnenguaji wa Extra Bongo.

Na Princess Asia
BENDI ya muziki wa dansi ya Extra Bongo na kundi la taarabu la Jahazi Modern ndiyo burudani zitakazonogesha tamasha la vyombo vya habari litakalofanyika Dar es Salaam keshokutwa.
Akizungumza Dar es Salaam leo, wakati wa kutambulisha burudani hizo, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinachoandaa bonanza hilo, Juma Pinto alisema maandalizi kuhusiana na tamasha hilo linalojulikana kama Media Day Bonanza yamekamilika.
Alisema wameichukua Extra Bongo inayoongozwa na Ally Choki na Jahazi Modern inayoongozwa na Mzee Yusuph kutokana na makundi hayo kuwa juu hivi sasa katika muziki kwa maeneo yao.
“Tunaamini watakaokuja kwenye tamasha watakuwa na furaha ya aina yake na tumejiandaa vya kutosha,” alisema Pinto na kueleza kuwa bonanza hilo litafanyika viwanja vya Sigara Chang’ombe, Dar es Salaam na mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
Pia Pinto alisema bendi ya Msondo Ngoma Music itapiga kwenye viwanja hivyo kuanzia saa moja usiku baada ya bendi za Extra Bongo na Jahazi kumaliza kutumbuiza Media Day na kwamba imetoa ofa kwa wanahabari watakaotaka kubaki kuendelea kupata burudani mpaka usiku wa manane.
“Msondo wana bonanza lao kila Jumamosi, sasa wamekubali kwamba wanahabari watakaotaka kubaki baada ya bonanza kumalizika jioni wabaki wajiunge na Msondo Ngoma,” alisema Pinto.
Bonanza hilo la TASWA linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) likiwa na lengo la kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari ili kubadilishana mawazo na kufurahi pamoja.
Kwa upande wake Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu alisema wamejipanga vya kutosha na kwamba wadau wafike kwa wingi kuhakikisha mambo yanaenda kama yalivyopangwa.
“TBL ni mdau mkubwa wa wanahabari, tumewaandalia mambo mazuri, naomba msikose,” alisema Malulu na kuongeza kuwa wanaamini wadau 1,500 kutoka vyombo mbalimbali vya habari wanaotarajiwa kushiriki bonanza hilo watafurahi vya kutosha siku hiyo.
Naye Choki akizungumza kwenye mkutano huo, alisema vijana wake wamejipanga vya kutosha kushambulia na kuwa dhamira yao ni kuona wana habari wanafurahi vya kutosha na kuwa mambo waliyowaandalia kila mtu atafurahi kuiona Extra Bongo.
Ally Choky katikati, kulia Nyamwela na kushoto Dorris

Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto (katikati) akizungumza. Kushoto ni Katibu, Amiri Mhando na kulia Dorris

Dorris katikati akizungumza

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI