JK AFUNGA SEMINA YA MFUMO MPYA WA KUSIMAMIA UTEKEREZAJI, UFUATIRIAJI NA TATHMINI YA MIRADI YA MAENDELEO
Rais Jakaya Kikwete akifunga semina kwa mawaziri na makatibu wakuu walioketi na kupanga mikakati ya utekelezaji wa mfumo mpya wa kusimamia utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo katika ukumbi wa St Gaspar mjini Dodoma leo. Mfumo huo unaanza kutekelezwa kwa kutumia uzoefu wa Performance Management and Delivery Unit (PEMANDU) ya Malaysia. Mfumo huu utajumuisha uanzishwaji wa taasisi ya President’s Delivery Bureau (PDB) ambayo itafanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Katika mfumo huu, uchambuzi wa kina wa kimaabara (labs) utafanyika ili kuandaa programu za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Awamu ya kwanza ya labs ilizinduliwa rasmi na Rais Kikwete Februari 22, mwaka huu na kukamilika Aprili, 2013. Maeneo ya awamu ya kwanza ya labs yanahusisha elimu, kilimo, nishati, mapato, maji na miundombinu ya uchukuzi.
Comments