KESI ILIYOFUNGULIWA NA MWANDISHI MKONGWE KUPINGA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI KUANZA KUNGURUMA APRILI 17 JIJINI DAR ES SALAAM

Mwandishi  mkongwe wa kujitegemea, Timothy Kahoho (kulia), akionesha kitabu cha makubaliano ya kuanzishwa kwa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), kichosainiwa Novemba 30, 1999 jijini Arusha,  wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu kesi aliyofungua dhidi ya Katibu Mkuu wa Jumuia hiyo,  Dk. Richard Sezibera ambayo itaanza kusikilizwa Aprili 17, mwaka huu katika Mahakama ya Biashara Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa wa Idara Habari Maelezo, Hussein Makame.

Na Dotto Mwaibale

KESI namba 1/2012 iliyofunguliwa na Mwandishi mkongwe wa kujitegemea Timothy Kahoho dhidi ya Katibu Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki Dk. Richard Sezibera itaanza kusikilizwa Aprili 17 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Shauri hilo linahusu tamko lililotolewa na wakuu wa nchi wanachama wa nchi za Afrika Mashariki katika mkutano uliofanyika Bujumbura Burundi.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam mlalamikaji katika shauri hilo Timoth Kahoho alisema kesi hiyo yenye madai manne itasikilizwa na jopo la majaji watano.

"Kesi hii ya aina yake itasikilizwa na jopo la majaji watano na itatoa fursa ya kusikilizwa na kuonwa na wananchi wa jumuia hiyo na nchi nyingine mbalimbali kutokana na kufungwa mitambo maalumu ya kuonesha kila kitakachokuwa kikiendelea chumba cha mahakama" alisema Kahoho.

Aliwataja  majaji hao kuwa ni Jaji Kiongozi Johnson Busingye, Naibu Jaji Kiongozi Mary Stellah Amoko, Jaji John Mkwawa, Jaji Jean Bitasi na Jaji Isaac Lenaola.


Kahoho alisema dai la kwanza ni kikao hicho cha wakuu wa nchi hizo kupitisha itifaki ya kinga kwa mtumishi wa jumuia, vitengo vyake na taasisi zake kwamba ni kukiuka ibara ya 73, 138 ya makubaliano ya nchi zilizopo katika jumuia hiyo.

Alisema dai jingine  ni kikao hicho cha wakuu hao kuelekeza sekretarieti kuhusu mambo yanayohusu umoja wa forodha, soko la pamoja na sarafu moja na mchakato wa wa muundo wa shirikisho la jumuia ya Afrika Mashariki kwamba ni kukiuka ibara ya 6,7 na 123 (6) ya makubaliano ya nchi zilizomo katika jumuia hizo.

Alisema kesi hiyo ilifunguliwa jijini Arusha januari 20 mwaka 2012 ambapo imepanga kusilizwa katika moja ya chumba cha Mahakama Kuu ya Biashara jijini Dar es Salaam tarehe hiyo.

Alisema mkutano uliopitisha tamko hilo chini ya katibu huyo ulifanyika novemba 30 mwaka 2011 Bujumbura Burundi na kuhudhiriwa na Mwenyekiti wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya, Rais wa Burundi Pierre Nkuruzinza, Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal na Waziri Mkuu wa Rwanda Pierre Habumulemyi.

Alisema kesi hiyo itakuwa ya kihistoria kwa kuwa ya kwanza kupinga tamko la wakuu wa jumuia  hiyo ya Afrika Mashariki.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.