Kinana amaliza ziara yake morogoro vijijini,akagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza
Meneja Mradi wa mashamba ya Mfano ndani ya kijiji cha Pangawe,wilaya ya
Morogoro vijijini,Bwa.Kim Sun Ho wa KOICA walipokuwa wakitembelea
Shamba hilo lenye Wakaazi wapatao 180,ambao wanasimamiwa na kupewa
mafunzo ya Kilimo cha kisasa na ufugaji bora kutoka kwa shirika la
Maendeleo la Korea (KOICA).
Kinana
na Ujumbe wake wa chama hicho walitembelea mradi huo katika ziara yao
ya kichama,Wakaazi hao wanamiliki zaidi ya hekari 150 kila mmoja ana
magunia nane ya mahindi waliyovuna mwaka jana huku wakiwa na na kiasi
cha shilingi milioni 50 benki.CCM imefanya ziara katika Wilaya ya
Morogoro vijijini na kufungua mashina na matawi ya chama hicho huku
akipokea wanachama wapya waliojiunga na waliotoka vyma vya upinzani.
Sehemu ya Shamba la mfano la Mahindi.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Ndugu Abdulrahman Kinana akipata
maelezo mafupi kutoka kwa Meneja Mradi wa KOICA,Bwa.Kim Sun Ho wa
KOICA,alipotembelea mradi wa majengo yatakayotumika katika mafunzo ya
ufugaji wa kisasa katika kijiji cha Pangawe,Wilaya ya Morogoro Vijijini.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akijadili jambo na Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM,Nape Nnauye walipotembelea mradi wa majengo yatakayotumika katika mafunzo ya ufugaji wa kisasa katika kijiji cha Pangawe,Wilaya ya Morogoro Vijijini.
Pichani
ni Sehemu ya soko la Kisasa la Mkuyuni linalojengwa na CCM kwa gharama
ya shilingi milioni 100,katika kata ya Mkuyuni,ndani ya Morogoro
Vijijini.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurlhaman Kinana akiangalia kazi za ujasiliamali
zinazofanywa na mkazi wa kijiji cha Makuyuni,Mkaazi huyo ameamua
kujiajiri kuwa kutengeneza mafagio ya njiti na kuyauza kwa wananchi wa
eneo hilo,kwa ajili ya kujiongezea kipato.
Ndugu Kinana na ujumbe wake wa CCM wakielekea kukagua ujenzi unaoendelea wa kituo cha afya (zahanati) ya Mkuyuni.
Ujenzi wa jengo la kituo cha zahanati ya Mkuyuni ukiendelea .
Mmoja
wa Wahudumu wa kituo cha afya cha Mtamba-Matombo wilaya ya Morogoro
Vijijini, kilichopandishwa hadhi na kuwa Zahanati,Bi.Lilian Peter Haule
akitoa maelezo mafupi ya maendeleo ya upanuzi wa ujenzi wa zahanati
hiyo ya Mtamba kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurlhaman Kinana.
Ndugu Kinana akikamkabidhi kadi mpya,katibu kata wa Kiroka kutoka chama cha CUF,Hadim Omary,Wilaya ya Morogoro Vijijini.
Mwenyekiti
wa CHADEMA kata ya Kiroka akikabidhi kadi na bendera ya chama hicho kwa
Ndugu Kinana,na kuwapokea kama wananchama wapya wa chama cha CCM na
kuwakabidhi kadi mpya.
Wakazi
wa Kata ya Kiroka,wakishngilia jambo walipokuwa wakimsikiliza Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman alipozungumza nao mara baada ya kuzindua
jiwe na la msingi la ofisi hiyo.
Katibu
tawi la Gumba kutoka chama cha CUF,Said Almas akirejesha kadi yake ya
na kupokea kadi mpya ya CCM,akijiunga kuwa mwananchama mpya kutoka kwa
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrhman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Abdurlhaman Kinana akipewa zana za kimila kutoka kwa Chifu Kingaru wa kabila la
Waruguru .
Wananchi wa Kata ya Mvuha-Matombo
wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi wa CCM Nape Nnauye,aidha
Ndugu Kinana na ujumbe wa CCM umehitimisha ziara yake ya Morogoro vijijini na
leo wataunguruma Morogoro mjini ikiwemo pia kukagua maendeleo ya miradi ya mbalimbali ya chama
hicho ikiwemo na kukiimarisha chama.
Comments