MAMA SALMA KIKWETE APEWA NISHANI YA KAZI ZA WAMA KUTOKA TAASISI ILIYOPO LONDON, UINGEREZA

Naibu Spika Mh. Job Ndugai na Mbunge Mama Beatrice Shelukindo wakipokea nishani hiyo kutoka kwa Dr Mohammed Zaharani (katikati yao )  kwa niaba ya Mama Salma Kikwete .  Pembeni wa kwanza ni Nd. Haruna Mbeyu maarufu kama Meya wa London na anaefuatia kabla ya Mh. Mama Shelukindo ni Bi. Mariam Mungula , Katibu wa Tanzania Women Association (TAWA) UK.
Mh. Naibu Spika Job Ndugai akipokea Nishani hiyo kutoka kwa Dr. Mohammed Zaharani . Wakiangalia kwa furaha ni Mh. Beatrice Shelukindo, Bi Mariam Mungula na Nd. Haruna Mbeyu.

Baadhi ya Akina Mama waKitanzania waliohudhuria hafla hiyo katika picha ya upendeleo na M. Beatrice Shelukindo na Nishati ya Mama Salma.

LONDON, Uingereza
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mwanaharakati wa Kijamii kupitia Chama Chake cha Wanawake na Maendeleleo, wiki iliyopita alizawadiwa Nishani na Chama kinachojishughulisha na kuinua kiwango cha Elimu kwa Nchi za Afrika Mashariki kilichoko katika jiji la London, Uingereza.
Akiongea katika Hafla hiyo fupi iliyofanyikia katika kumbi za Hoteli ya Park Plaza iliyopo pembeni mwa Westminster Bridge (katikati ya jiji la London) Dr Mohammed Zaharan ambae ni Katibu wa Chama hicho cha East Africa Education Foundation (EAEF) alisema kuwa Chama Chake kimekuwa kikifuatilia kwa ukaribu na  shughuli zinazofanywa na Mama Kikwete kupitia Jumuiya ya WAMA na wamefurahi kupata
fursa hii ya kumtunukia "Award" kwa mchango wake mkubwa sana wa kuinua Elimu ya Mtoto, hususan wa kike na vilevile kuwezesha Wanawake ili waweze kujitegemea. Dr Zaharani aliongeza kuwa Mama Kikwete ni mfano bora sana wa kuigwa na Wanawake katika jamii ndani na nje ya Tanzania.
Akipokea Nishani hiyo kwa Niaba ya Mama Salma Kikwete, Naibu Spika Mh. Job Ndugai  (Ambae alikuwa Nchini Uingereza kwa Mualiko wa Naibu Spika wa Uingereza na aliongoza na Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Utumishi ya Bunge) alisema kuwa amefurahishwa sana na kitendo hicho cha Mchango wa Mama Salma kuonekana, kwa kuwa kinadhihirisha mchango unaofanywa na Jumuiya zisizo za Kiserikali katika jamii kama WAMA unaonekana mpaka Nje ya Tanzania.
Nae Mh. Mama Beatrice Shelukindo alifurahi zaidi kwa kitendo hiki na kusema kuwa hili ni jambo kubwa sana na linadhihirisha mchango mkubwa wa Mama Salma katika kumuendeleza Mwanamke wa KiTanzania na inatoa moyo kwa Wanawake Wengine.
HONGERA SANA MAMA SALMA NA MWENYEZI MUNGU AZIDI KUKUONGOZA NA KUKUPA AFYA NJEMA ILI UWEZE KUCHANGIA ZAIDI KATIKA MAENDELEO YA MWANAMKE NA MTOTO WA KIKE.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA