Messi aizamisha AC Milan


Mshambuliaji wa Barcelona,Lionel Messi akifunga bao lake la pili dhidi ya AC Milan wakati wa mechi ya Ligi ya Mabingwa iliyozikutanisha timu hizo kwenye Uwanja wa Camp Nuo.Barcelona ilishinda 4-0.  


Barcelona, Hispania
Mabao ya Lionel Messi na David Villa yalitosha kuipa Barcelona ushindi mnono wa 4-0 na kuibwaga AC Milan kwa jumla ya mabao 4-2  kwenye Uwanja Camp Nou.

Kwa ushindi huo Barca imeungana na Juventus, Real Madrid na
Galatasaray iliyolazimisha sare 2-2 na Schalke 04  kwenye Uwanja Auf Schalke na kusonga mbele kwa sheria ya bao la ugenini baada ya mchezo wa kwanza kumalizika kwa sare 1-1 hivyo kufuzu kuingia robo fainali.

Messi ameendeleza rekodi yake kwa kufunga mechi 18 mfululizo, baada ya kuifungia Barca katika dakika 5 na 40, kabla ya Villa na Jordi Alba kupachika mabao mengine mawili.

 

Washambuliaji wa Milan,  Stephan El Shaarawy na M'Baye Niang walipoteza nafasi kadhaa za kufunga katika mchezo huo na kuinyima timu mabao.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU