MGEJA AWATAKA VIJANA KUWAPUUZA WANASIASA WANAOHUBIRI MAANDAMANO

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM), Khamis Mgeja (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanachama wa Tawi la Wakereketwa la Pamba Road, katikati ya Jiji la Dar es Salaam jana. Aliyevaa koti ni Mwenyekiti wa tawi hilo, Ramadhan Makula ambaye alimwalika Mgeja kutembelea tawi lao. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

Na  Mwandishi Wetu

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (NEC), Khamis Mgeja, amewataka vijana wawapuuze wanasiasa wa vyama vya upinzani wanaohubiri maandamano, badala yake wajikite katika kufanya kazi kwa bidii kwani ndiyo ni njia pekee ya kujiletea maendeleo.

Mgeja ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Shinyanga, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na vijana wa Tawi la Pamba Road, Dar es Salaam ambao  walimkaribisha kumweleza changamoto wanazokabiliana nazo.

Alisema wanasiasa wa vyama vya upinzani wamekuwa wakipandikiza chuki miongoni mwa wanajamii kwa kuwaambia kuwa eti Serikali inaweza kuwatafutia ajira wakati tatizo hilo ni la dunia nzima na kwamba suluhisho ni kufanya kazi kwa bidii.

"Wapuuzeni wanasiasa wanaopandikiza chuki. Matatizo haya ya ajira lazima tuyakabili kwa kufanya kazi kwa bidii,"alisema Mgeja.

Aliongeza kuwa matatizo ya vijana yanazungumzika na si kauli za viongozi hao kuwaambia wananchi kuwa wanawashtakia viongozi kwao waamue cha kuwafanya hatua ambayo inaeneza taifa lenye manung'uniko.

Alibainisha kuwa Serikali ya CCM inafahamu matatizo mbalimbali waliyonayo wananchi wake ndiyo maana inasisitiza watu wafanye kazi kwa bidii na kuhimiza mabenki yawakopeshe wafanyabiashara wadogo.

Aliwasifu vijana wa tawi hilo kujikita katika kazi mbalimbali za ujasiliamali wakiwemo mafundi viatu.

Aliwataka waendelee kujikita katika kazi za kujiongezea kipato badala ya kupanga uhalifu ambao hauleti taswira njema katika jamii.

Aidha kiongozi huyo wa Chama Cha Mapinduzi, Mkoa Shinyanga, alitoa msaada wa sh. 100,000 kwa vijana hao ili ziwasaidie kununua rangi za kupaka katika viatu.



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.