Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kulia), akikata utepe kuzindua rasmi jukumu la kuwasafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Dodoma. Katikati ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mary Shangali, kushoto ni Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Dk.Eliezer Feleshi ambao walikuwa katika uzinduzi huo uliofanyika katika Gereza Kuu Isanga Dodoma.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, akiwasha moja ya magari yaliyozinduliwa kuashiria uzinduzi wa kuwasafirishia Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Dodoma. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Isanga Dodoma.
 Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua mabasi mawili na gari ndogo moja (pick-up) kwa ajili ya kuwasafirishia mahabusu toka gerezani kwenda mahakamani na kurudi gerezani kwa Mkoa wa Dodoma. Katika hotuba yake mkuu wa jeshi hilo aliwataka maofisa magereza wa mkoa huo wawe makini kuyatunza magari hayo. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Dodoma.

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akisalimiana na  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mary Shangali baada ya uzinduzi wa mabasi mawili na gari ndogo moja (pick-up). Kushoto Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Dk.Eliezer Feleshi. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Dodoma.
Magari matatu ya kuwasafirisha Mahabusu yaliyozinduliwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, katika hafla iliyofanyika Gereza Kuu Isanga Dodoma.


PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.