MTUHUMIWA MWINGINE WA ULIPUAJI WA MABOMU JIJINI BOSTON AKAMATWA

Maafisa waliomsaka Dzhokar Tsarnaev, mshukiwa aliyenaswa Ijumaa usiku mjini Boston Aprili 19, 2013.
Maafisa waliomsaka Dzhokar Tsarnaev, mshukiwa aliyenaswa Ijumaa usiku mjini Boston Aprili 19, 2013.

Baada ya siku tano za hofu kuu kwa wakazi wa Boston, jimbo la Massachusetts na vitongoji vyake, polisi walimkamata mshukiwa wa pili kufuatia milipuko ya mabomu wakati wa mashindano ya riadha mjini humo Jumatatu.

Mshukiwa huyo Dzhokhar Tsarnaev mwenye umri wa miaka 19 yumo chini ya ulinzi mkali wa polisi  Jumamosi katika hospitali ya Beth Israel Deaconess Medical Center mjini Boston, ambapo yaripotiwa kuwa yuko katika hali mahtuti.


Kakake mwenye umri wa miaka 26 Tamerlan aliuawa katika makabiliano ya risasi na polisi Alhamis usiku huku Dzhokar akitoroka kwa mguu.

 Baada ya msako mkali Ijumaa hatimaye polisi walimpata Tsarnaev akiwa amejificha kwenye boti nyuma ya nyumba moja katika kitongoji cha Watertown  mjini Boston. Maafisa wanasema alijisalimisha baada ya kufyatuliana risasi na polisi.

Mara baada ya habari za kukamatwa kwake, wakaazi wa Boston walijitokeza mjini kusherehekea na kupongeza juhudi za polisi na wote waliohusika  katika msako huo  wakiwemo maafisa wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai FBI. Baada ya taarifa hizo rais wa Marekani  Barack Obama aliwapongeza wote waliohusika na msako huo  akisema juhudi zao ni dhahiri kuwa Marekani imekataa kuhangaishwa na magaidi. 

Source: VOASWAHILI

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.