PPF YATIMIZA MIAKA 10 FAO LA ELIMU


Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Mama Salma Kikwete, akikabidhi zawadi ya kompyuta mpakato kwa mmoja wa wanafunzi waliopata daraja la kwanza katika matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2012 wakati wa sherehe za kuadhimisha mika 10 ya Fao la Elimu la Mfuko wa Pensheni jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.  Katikati anayeshuhudia ni Mweyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Adolf Mkenda. (Picha na Habari Mseto Blog) 
Na Mwandishi Wetu
MKE wa Rais  Salma Kikwete  ameomba  Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi (PPF)  kupitia Fao la Elimu  kuwasomesha watoto mpaka kidato cha sita ili kuweza kuwafanya watoto hao wasikatishe masomo kutokana na kukosa karo .
Salma aliyasema jana wakati wa maadhimisho ya miaka 10 Fao la Elimu linalotolewa na Mfuko wa Pensheni kwa watumishi (PPF),alisema kuwa fao hilo kuwasomesha mpaka kidato cha nne kuna uwezekano wa kukosa kuendelea na kidato cha tano na sita kutokana kukosa karo kwa walenzi inayosababishwa na kipato kuwa chini.
Alisema kuwa juhudi ambazo zimeonyeshwa na PPF kupitia fao la elimu kwa kuwasomesha watoto waliofiwa na wazazi ambao ni wanachama kumesaidia kuokoa ndoa kwa wasichana wadogo ambapo wasingeweza kuendelea na elimu kutokana na familia kuwa na kipato kidogo au kukosa kutambua fursa ya elimu kwa mtoto wa kike.
Salma alisema kuwa ni muhimu kwa mifungo mingine ya hifadhi ya Jamii kuanzisha utaratibu wa fao la elimu watakuwa wamesaidia sana katika kusuka gurudumu la elimu kwa watoto ambao wanaweza kuondokewa na wazazi wakiwa umri wao haujafikia kujitegemea.
Aliongeza kuwa kusomesha watoto 1333 katika utaratibu wa fao hilo wamesaidia kuweza kuleta chachu ya elimu kwa familia hizo na kusinge kuwepo kwa utaratibu huo wengine wasingeweza kusoma jamii inayochiwa kuona suala la  kusomesha watoto ambao wamefiwa na wazazi wao sio jukumu la lao.
Salma Kikwete aliwataka watoto wanaosomeshwa kupitia fao hilo kujituma na kuja kuwa nguvu kazi ya taifa yenye tija ya kuzalisha kupitia elimu ambayo wameipata kutokana na mwanga ulionyeshwa na PPF.
Mwenyekiti wa Bodi wa PPF Profesa Adolfu Mkenda alisema changamoto kubwa katika fao la elimu ni baadhi ya watu kupeleka watoto wao na kuachwa watoto waliofiwa na wazazi ambao ni wanachama wa mfuko huo.
Alisema kuwa watu ambao wanakuwa wamepewa jukumu la kusimamia familia ya marehemu ambaye ni mwanachama wa PPF ambapo wanatumia fursa ya kupeleka watoto wao na kuwaacha wahusika wa kupata haki hiyo.
mwisho  

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*