Rais Kikwete amteua tena Mhandisi Baya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC

Na Hussein Makame -Maelezo

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua kwa mara ya pili Mhandisi Bonaventure Baya (pichani), kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Hifadhi na Msimamizi wa Mazingira Nchini (NEMC) .

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Tutubi Mangazeni, Mhandisi Baya atatumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka mitano.

Pamoja na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Mhandisi Baya pia ni Rais wa kwanza wa Baraza la Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Ardhi na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Wataalamu wa Mazingira nchini.

Nyadhifa nyingine alizowahi kuzishika kabla ya uteuzi huo ni pamoja na  Mjumbe wa Bodi ya Taasisi ya Huduma ya Misitu na Mjumbe wa Bodi ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Aidha Mhandisi Baya amewahi pia kuwa Mjumbe wa Bodi ya  Wizara ya Kilimo na Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Hifadhi ya Misitu ya Milima ya Mashariki (TAO).

Uteuzi huo umeanza tangu Oktoba 08 mwaka 2012 ambapo Mhandisi Baya anatarajia kutumikia cheo hicho hadi mwezi  wa kumi  mwaka 2017.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.