RAIS KIKWETE, MAMA SALMA KIKWETE WAHUDHURIA DHIFA YA KITAIFA YA KUMPONGEZA KENYATTA

 Rais Jakaya  Kikwete akimpongeza Rais Mpya wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta huko Ikulu mara baada ya kuapishwa rasmi kuwa rais wa nne wa nchi hyo katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa kimataifa wa michezo wa Moi-Kasarani jijini Nairobi tarehe 9.4.2013.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais aliyemaliza muda wake Mheshimiwa Mwai Kibaki huko ikulu jijini Nairobi mara tu baada ya sherehe ya kumwapisha Rais Mpya wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru  Kenyatta kumalizika huko uwanja wa Moi Kasarani tarehe 9.4.2019

  Rais wa Kenya  aliyemaliza muda wake, Mheshimiwa Mwai Kibaki akifanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma huko Ikulu mara baada ya sherehe ya kumuapisha rais mpya wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta kukamilika.

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mama Magrate  Kenyatta katika ikulu ya Kenya  jijini Nairobi mara baada ya sherehe za kuwaapisha kukamilika.

  Rais Jakaya  Kikwete akizungumza na Rais Mpya wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta huko Ikulu mara baada ya kuapishwa rasmi kuwa rais wa nne wa nchi hyo katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa kimataifa wa michezo wa Moi-Kasarani jijini Nairobi tarehe 9.4.2013
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na wake wa viongozi wa juu wa Kenya, Mama Magrate Kenyatta (kushoto) ambaye ni mke wa Rais Uhuru na Mama Recheal  Ruto (kulia) Mke wa Naibu Rais wa nchi hiyo Mheshimiwa William Ruto huko ikulu jijini Nairobi mara tu baada ya kuapishwa  viongozi hao tarehe 9.4.2013.

 Marais Jacob Zuma wa Afrika Kusini (kushoto), Rais Jakaya Kikwete na         Bongo wa Gabon wakifanya mazungumzo kwenye ikulu ya Nairobi mara baada ya kumalizika sherehe ya kuwaapisha viongozi wakuu wa Kenya zilizofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Moi Kasarani tarehe 9.4.2013.

 Baadhi ya Marais na wakuu wa nchi wakiwa na wake zao katika picha ya pamoja huko ikuku jijini Nairobi baada ya kumalizika sherehe ya kumwapisha rasmi Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto.

  Rais Jakaya Kikwete kwa niaba ya viongozi wengine waliohudhuria sherehe za kuapishwa viongozi wapya  akimshukuru Rais Uhuru Kenyatta na wananchi wa  Kenya kwa kufanikisha uchaguzi na sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa nchi hiyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.