RC LINDI AZINDUA MPANGO MAALUM WA HUDUMA ZA MATIBABU KWA MADAKTARI BINGWA UNAORATIBIWA NA NHIF

Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa akisoma hotuba fupi wakati wa uzinduzi wa mpango maalum wa huduma za matibabu ya madaktari bingwa kwa wanachama na wananchi mkoani humo na kuwataka wajitokeze kwa wingi na kuenzi huduma hiyo kwani itaokoa maisha ya wengi,kulia ni mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Dk. Hamid Nassoro (kushoto) kwake ni Mkurugenzi wa NHIF wanaofatia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Dk. Yusuf Sonda na Dk. Frank Lekey wa NHIF.

Mgeni rasmi Mhe. Abdallah Ulega kaimu mkuu wa mkoa wa lindi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa huduma za matibabu ya madaktari bingwa sambamba na kupokea dawa na vifaa tiba kutoa nhif ili kufanikisha zoezi ilo wanaoshuudia kulia ni mkuu wa wilaya ya lindi Mhe. Dr Hamid Nassoro,kaimu RAS Lindi Ndg John Likango na kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya, Bw. Emanuel Humba

Wanachama na wananchi waliojitokeza wakimsikiliza mgeni rasmi hayupo pichani kwenye viwanja vya Hospitali ya Mkoa (Sokoine) Lindi.

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Emanuel Humba akitoa ufafanuzi wa umuhimu wa utekelezaji wa mpango huo maalum uliobuniwa na mfuko kwa kutoa huduma za madaktari bingwa kwenye mikoa iliyo pembezoni,na kuzinduliwa mkoani Lindi.
******************************************
NHIF  YAANZISHA KAMPENI YA HUDUMA YA  MATIBABU YA MADAKTARI BINGWA KWENYE MIKOA YA PEMBEZONI

Wanachama na wananchi mkoani Lindi wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kutumia vyema fursa za huduma za madakatri bingwa zinazoratibiwa na mfuko wa taifa wa bima ya afya  katika hospitali ya mkoa sokoine.

Hayo  yalisemwa na mgeni rasmi  kaimu mkuu wa mkoa wa Lindi ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Kilwa mhe: Abdallah Ulega  wakati wa uzinduzi wa mpango maalum wa utoaji  huduma za matibabu kwa madaktari bingwa kutoka hospitali ya taifa muhimbili kwa magonjwa ya  akinamama,wataalam wa upasuaji na magonjwa ya  moyo,figo na shinikizo la damu  uliofanyika katika viwanja vya hospitali ya sokoine mjini lindi

Ulega alisema ni fursa adhimu ambayo wengi wetu hapa mkoani Lindi,hatukuwahi kukutana nayo na sababu kubwa inawezekana ni uwezo wa kugharamia safari ya kwenda huko wanakopatikana madaktari bingwa sanjari na mlolongo mrefu wa taratibu za kitabibu ili kuwafikia,lakini wenzetu, yaani bodi ya wakurugenzi, menejimenti  ya Mfuko wa taifa ya bima ya afya wameiona changamoto hii na niseme wazi kuwa mpango huu utakuwa unaokoa maisha ya watu wengi ambao hawakuwahi wala kuwa na ndoto za kukutana na madaktari bingwa katika maisha yao.

Huduma hizi zimepangwa kufanyika kwa siku saba hapa hospitalini kwetu  Sokoine mkoani Lindi, hivyo nawaomba madaktari wetu tutakaoshirikiana na hawa madaktari bingwa tujifunze kwa maana ya kujiongezea ujuzi wa kitabibu ili watakapoondoka huduma hizi zisitetereke bali ziboreke zaidi,hivyo wanachama na wanachi wa mkoa wa Lindi na Mtwara wafike hapa kupata matibabu bora na stahiki.alisisitiza mhe ulega.

Pia aliwataka wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii(CHF) ili waweze kunufaika kwa kupata matibabu mhe ulega alisema…Maradhi hayabishi hodi wananchi hivyo kwa kuchangia CHF uhakika wa matibabu ni mkubwa na pia  utachochea maboresho ya huduma za matibabu kwenye vituo vya afya,zahanati hadi hospitali mkoa wetu.

Naye mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa taifa wa bima ya afya ndg Emanuel Humba alisema mpango huu maalum wa kupeleka huduma za madaktari bingwa  kwenye  mikoa ya pemebezoni , umezingatia mahitaji ya msingi na ya wakati kwani ni dhairi wapo wanachama wetu wengi waliopo vijijini,wana mahitaji makubwa ya huduma za madaktari bingwa pasipo kuzipata kwa wakati.

Tunatarajia pia kufanikiwa kwa mpango huu kutapunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali kubwa,hivyo kutoa fursa kwa madaktari hao kutoa huduma kwa uhakika zaidi sanjari na kuibua ukubwa wa mahitaji ya huduma za madaktari bingwa hapa mkoani lindi na nchi kwa ujumla.

Alisema Mfuko umewagharimia madaktari hao pamoja na utoaji wa dawa na vifaa tiba ,ili kufanikisha mpango huo wenye thamani zaidi ya  millioni hamsini,na  mpango huu maalum utekelezaji wake  umeanzia  mkoani Lindi na utakuwa ukitekelezwa kila baada ya miezi mitatu na wanachama wa Mfuko watapata matibabu kwa kutumia kadi zao sambamba na  wananchi watapata huduma kwa kupitia utaratibu wa kawaida ambao utakuwa na nafuu  

Alihitaja Mikoa ambayo iko kwenye mpango huu maalum ni Kigoma,Rukwa,Katavi,Mara ,Pwani na Tabora,hivyo wanachama na wananchi kwa ujumla wajitokeze ili waweze kutumia fursa hii muhimu na adimu kupata huduma za matibabu za madaktari bingwa.
You might also like:

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.