Sekondari kongwe Ndanda taabani

b009 
Na Mwandishi Wetu
WADAU wa elimu nchini waliopitian katika shule kongwe ya Sekondari yaNdanda, wilayani Masasi, mkoani Mtwara wameombwa kuisaidia kwa hali na
mali shule hiyo ambayo kwa sasa baadhi ya miundombinu yake iko katika
hali mbaya.
Hayo yameelezwa hivi karibuni na Morega Mongate, Mkuu wa Shule hiyo
iliyoanzishwa Julai mwaka 1928, ikimaanisha kuwa mwaka huu inatimiza
umri wa miaka 85. Na katika kipindi hicho, imebahatika kutoa wasomi
mahiri na watu mashuhuri, akiwemo Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu,
Benjamin Mkapa.
Mongate alisema kuwa, miongoni mwa matatizo sugu katika shule hiyo ni
pamoja na kukosekana kwa maabara ya uhakika, uchakavu wa mabweni, jiko
na hata maktaba ambayo ina uhaba mkubwa wa vitabu, hasa vya sayansi.
Ingawa ilianza ikiwa na wanafunzi chini ya 200, lakini sasa wakifikia
zaidi ya 1,000 lakini kwa miundombinu ile ile, Mongate ameomba
ushirikiano wa karibu kutoka kwa watu waliosoma, waliowahi kufanya
kazi au kuguswa na matatizo ya elimu nchini kuweza kuinusuru shule
yake.
“Ni matatizo yanayohitaji utatuzi ili kuyafanya mazingira ya kusomea
na hata kulala kuwa rafiki zaidi, lengo likiwa kuinua uwezo wa
kitaalumu kishule kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
“Ndanda ina historia ya kipekee, imetoa watu mashuhuri na wasomi
mahiri, lakini kwa sababu dhamira yetu ni kuendelea kubakiza jina zuri
la Ndanda katika sekta ya elimu, tumeona ni vyema kero zilizopo
zikapatiwa ufumbuzi,” alisema Mongate.
Alisema kwa ujumla, kiasi cha sh milioni 135 kinahitajika ili kuipa
shule hadhi inayostahili, ikiwa pamoja na kufanya ukarabati mkubwa wa
mabweni likiwamo la kihistoria alilotumia Rais Mstaafu Mkapa, jiko na
ununuzi wa vifaa vya maabara na pia kuipa uhai maktaba.
“Kwa watakaoguswa wanaweza kuwasiliana nami kwa simu 0766 469 670.
Misaada mingine inaweza kutufikia shuleni au kupitia akaunti ya Mfuko
wa Maendeleo wa Shule ya Sekondari Ndanda yenye namba 7050 1200 175 ya
benki ya NMB, tawi la Masasi,” alisema.
Mbali ya Mkapa, wengine waliosoma shule hiyo ni pamoja na Waziri wa
Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Hawa Ghasia.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.