TCRA yakemea ukiukwaji wa matakwa ya sheria na kanuni za usajili wa namba za simu za mkononi.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prof. John Nkoma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutoa tamko la pamoja kwa umma la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na Makampuni yanayotoa Huduma za Simu kuhusu Usajili wa namba za Simu za Mkononi Tanzania ambapo amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ikishirikiana na makampuni ya Simu na vyombo vya usalama imeanza kampeni endelevu yenye lengo la kuwabaini wote wanaohusika na uvunjifu wa sheria ili kuwalinda watumiaji wema na jamii kwa ujumla kwa ajili ya kuimarisha usalama na kuleta maendeleo na ustawi wa wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania Diego Gutierrez akielezea jinsi kampuni yake ilivyojidhatiti katika kutoa huduma kwa wateja na kuhakikisha kila namba ya simu inayotolewa na kampuni ya simu ya Tigo inasajiliwa kwa mujibu wa kifungu cha 102 (1) cha Sheria ya mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma (wa tatu kushoto) akiwa meza kuu na Wakurugenzi Watendaji Wakuu wa Kampuni yanayotoa huduma za simu nchini.
Baadhi maafisa mbalimbali na wawakilishi wa makampuni yanayotoa huduma za simu nchini katika mkutano huo.
Sehemu ya wawakilishi mbalimbali wa vyombo vya habari nchini.
--
Na.Mwandishi wetu
Watumiaji, watoa huduma, wakala wa makampuni ya simu za mkononi na wananchi kwa ujumla wamekumbushwa kuwa ni kosa kisheria kutumia au kuwezesha kutumiwa kwa namba ya simu ambayo haijasajiliwa.
Akitoa tamko la pamoja kwa umma la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na Makampuni yanayotoa Huduma za Simu kuhusu Usajili wa namba za Simu za Mkononi Tanzania Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma amesema ni kosa la jinai kutumia namba ya simu isiyosajiliwa na adhabu yake ni faini ya shilingi laki 5 au kifungo cha miezi mitatu.
Ameongeza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 130 cha Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010, mtu yeyote ambaye anauza au anatoa kwa namna yeyote ile namba namba ya simu bila kuisajili anatenda kosa la jinai na adhabu yake ni faini ya shilingi 3,000,000 ai kifungo cha miezi 12 au vyote.
Aidha Prof. Nkoma amewashauri watumiaji wa simu za mkononi na wananchi kuunga mkono juhudi zinazofanywa ili kufanikisha usajili wa namba za simu kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta nay a Taifa kwa ujumla.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA