"TUTAWASHITAKI WATUMIAJI WA NAMBA ZA SIMU ZISIZOSAJILIWA"......TCRA
Watumiaji,
watoa huduma, wakala wa makampuni ya simu za mkononi na wananchi kwa ujumla
wamekumbushwa kuwa ni kosa kisheria kutumia au kuwezesha kutumiwa kwa namba ya
simu ambayo haijasajiliwa.
Akitoa tamko la pamoja kwa umma la Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania na Makampuni yanayotoa Huduma za Simu kuhusu Usajili wa
namba za Simu za Mkononi Tanzania Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma amesema ni kosa la jinai kutumia namba ya simu
isiyosajiliwa na adhabu yake ni faini ya shilingi laki 5 au kifungo cha miezi
mitatu.
Ameongeza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 130
cha Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010, mtu
yeyote ambaye anauza au anatoa kwa namna yeyote ile namba namba ya simu bila
kuisajili anatenda kosa la jinai na adhabu yake ni faini ya shilingi 3,000,000
ai kifungo cha miezi 12 au vyote.
Aidha Prof. Nkoma amewashauri watumiaji wa
simu za mkononi na wananchi kuunga mkono juhudi zinazofanywa ili kufanikisha
usajili wa namba za simu kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama
na kuharakisha maendeleo ya sekta nay a Taifa kwa ujumla.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania Prof. John Nkoma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa kutoa tamko la pamoja kwa umma la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania na
Makampuni yanayotoa Huduma za Simu kuhusu Usajili wa namba za Simu za Mkononi
Tanzania ambapo amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ikishirikiana na
makampuni ya Simu na vyombo vya usalama imeanza kampeni endelevu yenye lengo la
kuwabaini wote wanaohusika na uvunjifu wa sheria ili kuwalinda watumiaji wema na
jamii kwa ujumla kwa ajili ya kuimarisha usalama na kuleta maendeleo na ustawi
wa wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya simu za
mkononi ya Tigo Tanzania Diego Gutierrez akielezea jinsi kampuni yake
ilivyojidhatiti katika kutoa huduma kwa wateja na kuhakikisha kila namba ya simu
inayotolewa na kampuni ya simu ya Tigo inasajiliwa kwa mujibu wa kifungu cha 102
(1) cha Sheria ya mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) Prof. John Nkoma (wa tatu kushoto) akiwa meza kuu na Wakurugenzi
Watendaji Wakuu wa Kampuni yanayotoa huduma za simu nchini.
Baadhi maafisa mbalimbali na wawakilishi wa
makampuni yanayotoa huduma za simu nchini katika mkutano huo.
Sehemu ya wawakilishi mbalimbali wa vyombo
vya habari nchini.
SOURCE: DULLONET
Comments