VURUGU ZA NANI ACHINJE, DIWANI, MCHUNGAJI WAJISALIMISHA POLISI


DIWANI wa kata ya Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema na ) na Mchungaji wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Neema Benson Mwamafupa, jana walijisalimisha wenyewe polisi kwa ajili ya kutoa maelezo juu ya tuhuma za kuhusishwa na uchochezi wa vurugu zilizoibuka mjini humo.

Viongozi hao walijisamilisha kwa nyakati tofauti katika kituo cha polisi cha Mji mdogo wa Tunduma ambapo wote kwa ujumla walihojiwa na jeshi hilo kwa zaidi ya saa kumi, kabla ya kila mmoja kuachiwa.

Habari kutoka ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa wakwanza kujisalimisha katika kituo hicho cha polisi Tunduma alikuwa mchungaji Mwamafupa alijipeleka majira ya saa moja jioni hiyo juzi na kuhojiwa hadi majira ya saa nne usiku.

Wakati diwani Mwakajoka yeye alijisalimisha jana majira ya saa nne asubuhi akiwa ameandamana na baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Mbozi, ambapo naye alihojiwa kwa zaidi ya saa sita.

Juzi akitoa taarifa za vurugu hizo, Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani , alisema kuwa pamoja na chanzo cha vurugu hizo kuwa mgogoro wa kuchinja baina ya Wakristo na Waislamu, lakini kuna kila dalili za siasa kujipenyeza kutokana na taarifa za kiintelijensia kubaini kuwa wapo wanasiasa waliochoche vurugu hizo.

Alisema  kutokasna na taarifa za kiintelijensia kubaini kuwa wapo wanasiasa waliochoche vurugu hizo, aliwataka diwani wa kata hiyo, Mwakajoka na Mchungaji wa KKKT, … kujisalimisha badala ya kusubiri mpaka jeshi hilo liwakamate.

Mwakajoka alipotafutwa na Jambo Leo  kwa njia ya simu ili kuelezea tukio hilo, alikiri kujisalimisha polisi na kwamba alihojiwa kwa zaidi ya saa sita, ambapo awali alihojiwa na askari wa chini na baadae Ofisa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa (RCO).

“Ni kweli muda huu ni saa nane mchana bado niko hapa kituoni maana bnilifika hapa majira ya saa nne asubuhi na kuhojiwa na askari na hivi sasa wameniambia nimsubiri RCO (ofisa upelelezi makosa ya ninai mkoa)” alisema Mwakajoka.

Kwa upande wake, kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, akizungumza na waandishi wa habari  ofisini kwake jana, alisema hali katika mji wa Tunduma ilikuwa imeanza kurudi katika hali yake ya kawaida baada ya jeshi hilo kufanikiwa kuthibiti vurugu hizo.


Hata hivyo alisema, katika oparesheni endelevu iliyokuwa ikiendeshwa na jeshi hilo tangu  kuzuka kwa  vurugu hizo lilifanikiwa kukamata idadi zaidi ya wahusika wa vurugu hizo kutoka 40 hadi kufikia 65.

Shughuli za kiuchumi katika mji wa Tunduma na  mpakani wa Tanzania na Zambia jana zilisimama kwa zaidi ya saa kumi, kufuatia vurugu kubwa zilizoibuka ambazo chanzo chake kinadaiwa kuwa ni mgogoro  haki ya kuchinja baina ya Wakristo na Waislamu.

Vurugu hizo inadaiwa kuwa zilianza saa 3:00 asubuhi na kudumu hadi jioni huku baadhi ya vijana walijitokeza mitaani na kufunga bararabara kuu ya Tanzania na Zambia na kuchoma magurudumu ya magari pamoja na kurusha mawe hovyo,  hali ambayo ilisababisha askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kutumia nguvu ya mabomu ya machozi, risasi za moto na silaha nyingine kuwatawanya.

 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI