WATANZANIA WASHINDWA KUFANYA VIZURI KIPINDI CHA TANO CHA GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE

01Washindi wa kipindi cha tano cha Guinness Football Challenge Ken Muturi (kushuto) na Chris Mwamgi(kulia) wakishangilia ushindi walioupata huku wakiwa wamebeba pesa taslimu walizojishindia katika shindano hilo jana usiku na pembeni ni mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho Lary Asengo(anayepiga makofi kulia).
 ………………………………………………..
 Jana usiku kupitia Televisheni za ITV na Clouds TV timu ya Tanzania ilishindwa kutumia nafasi ya kipindi cha mwisho cha mashindano ya “Guinness Football Challenge” katika hatua ya Afrika Mashariki baada ya kutolewa na timu kutoka Kenya. Rangi nyekundu imeonekana kuwa ni rangi ya bahati kwa timu za Kenya kwani hii ni timu ya nne kutoka Kenya kufanikiwa kufuzu kuingia hatua ya Pan-African GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGETM. Kenneth Mukuri na Chris Mwamgi ndio walioibuka washindi jana usiku kwani walifanikiwa kufika katika hatua ya mwisho ya kulenga ukuta  wa pesa wa Guinness ambapo walijishindia dola za kimarekani  1,500. 

 Ni vipi Kenneth na Chris wataweza kumudu hatua ya Pan-African? Sasa wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano ya Pan-African ambapo watakutana na wawakilishi pekee kutoka Tanzania, Daniel Msekwa na Mwalimu, washiriki kutoka Uganda Alex Muyobo na Ibrahim Kawoova pamoja na wenzao kutoka Kenya,Francis Ngigi na Kepha Kimani(washindi wa kipindi cha 2), Kenneth Kamau na Wills Ogutu(washindi kipindi cha 3) na Ephantus Nyambura na Samuel Papa(washindi kipindi cha 4).
 Timu hizi tano zitakua uwanjani kutimiza malengo yao, ambapo watakutana uso kwa uso na washiriki kutoka Ghana na Cameroun kuonesha ni nani ana maarifa zaidi na ujuzi wa kusakata kabumbu,  hata kuvishwa ubingwa wa Pan-African na  kuondoka na dola za kimarekani 250,000.
 
 Usikose kuangalia mashindano haya kupitia televisheni za ITV na Clouds TV huku ukiburudika na kinywaji cha GUINNESS.
 
                              Tafadhali kunywa kistaarabu – Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.