WATU MILIONI 14 WANUFAIKA NA HUDUMA YA MATIBABU YA MABUSHA NA MATENDE TANZANA: DK. MWELE.
Na Mroki Mroki wa Father Kidevu Blog Arusha
Wilaya 94 zimefikiwa katika zoezi la unyweshaji dawa za Matende na Mabusha na utoaji elimu linaloendeshwa chini ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti magonjwa yasiyopea kipaumbele (NTD) unaoratibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Dakta
Mwelecele Malecela ameyasema hayo mjini Arusha wakati akizungumza na
waandishi wa Habari katika Kongamano la 27 la taasisi hiyo la Sayansi
la Kongamano la Pili la Afya Moja Afrika linaloendelea mjini humo.
Dk. Malecela amesema watu milioni
14 wamenufaika na huduma ya matibabu ya mabusha na matende katika
wilaya hizo 94 ambazo zimefikiwa katika zoezi la ugawaji dawa na tiba.
Aidha alieleza kuwa katika wilaya ya pangani jumla ya watu mia mbili waliokuwa wanasumbuliwa na mabusha wamepatiwa tiba kwa
njia ya upasuaji na tayari wamerejea katika hali ya kawaida na kuweza kuendelea na shughuli za maendeleo ya jamii yao.
njia ya upasuaji na tayari wamerejea katika hali ya kawaida na kuweza kuendelea na shughuli za maendeleo ya jamii yao.
Comments