XAVI AVUNJA REKODI YA PASI ULAYA, AWAFUNIKA WOTE UNAOWAJUA
HAKIKUWA kiwango bora kilichoonyeshwa na
Barcelona, lakini kwa Xavi ulikuwa ni usiku mzuri wa kuukumbuka:
akipatia kwa asilimia 100 katika pasi zake zote 96 alizopiga dhidi ya
Paris St Germain jana.
Vigogo hao wa Catalan walitolewa jasho
kupata nafasi ya kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa, walipokuwa
nyuma kwa bao 1-0 ndani ya dakika ya 50 na hatimaye kufuzu tu kwa faida
ya mabao ya ugenini, baada ya Pedro kusawazisha dakika ya 71.
Rekodi: Xavi alimfikishia kila pasi kila mchezaji mwenzake aliyempelekea jana dhidi ya Paris St Germain
Wengi watasifia kuingia kwa Lionel Messi
katikati ya kipindi cha pili kama siri ya mafanikio ya Barca jana,
lakini alikuwa ni Xavi aliyecheza kwa ubora wa hali ya juu katika nafasi
ya kiungo.
Tabasamu: Xavi akifurahia kwenye Uwanja wa Nou Camp jana na mchezaji mwenzake Andres Iniesta
Mspanyola huyo mwenye umri wa miaka, 33,
alikaribia kufunga dakika ya kwanza tu baada ya shuti lake la mpira wa
ashabu kudondokea nyuma ya nyavu na wengi uwanjani kudhani ni bao.
Alicheza dakika zote 90 katika mechi
hiyo na alifanikiwa kumfikishia pasi kila mchezaji mwenzake
aliyempelekea na kuwapiku wachezaji wengine wote kwa miaka 10.
Kazi nzuri ya Xavi jana kwa asilimia 100
anawapiku Javier Zanetti dhidi ya Tottenham miaka mitatu iliyopita na
nyota wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Eboue anayeshika nafasi ya tatu
katika orodha.
Lakini wakati Mspanyola huyo anamudu
kupiga pasi zake kwa asilimia 100, Zanetti na Eboue walipiga kwa usahihi
pasi 72 na 54 katika mechi zao.
Inafahamika uwezo wa Cristiano Ronaldo
unamfanya awepo katika orodha, lakini hamuachi mbali Nahodha wa Chelsea,
John Terry aliyefanya kazi nzuri dhidi ya Werder Bremen kwenye michuano
hiyo mwaka 2008.
Mkamate kama unaweza: Xavi alikuwa kila kitu Barca ikifuzu Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa jana
WAKALI WA PASI MURUWA LIGI YA MABINGWA TANGU MSIMU WA 2003/04
MECHI | MWAKA | MCHEZAJI | IDADI YA PASI |
---|---|---|---|
Barcelona v PSG | 2013 | Xavi | 96 |
Inter vs Tottenham | 2010 | Javier Zanetti | 72 |
FC Porto vs Arsenal | 2006 | Emmanuel Eboue | 54 |
Barcelona vs Stuttgart | 2007 | Lilian Thuram | 50 |
Real Madrid vs Man City | 2012 | Cristiano Ronaldo | 50 |
Braga vs Galatasaray | 2012 | Paulo Vinicius | 48 |
Basel vs Barcelona | 2006 | Martin Caceres | 48 |
Chelsea vs Werder Bremen | 2008 | John Terry | 47 |
FC Porto vs Dynamo Kiev | 2006 | Rolando | 45 |
Roma vs Real Madrid | 2004 | Ivan Helguera | 43 |
Real Madrid vs Dinamo Zagreb | 2011 | Sergio Ramos | 43 |
Comments