AKUTWA NA RUNDO LA KONDOMU TUMBONI

 https://encrypted-tbn1.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcSlAFE4zOGaQxD2hK_hJp2g4CMjt0S3DVrzwtIKD7S6RrZ0lXh-https://encrypted-tbn3.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcSoQP1u6_pGcSgoIrlHmZUekXe84Bf6l8ss8Lj9NsmSVuU7cQh1
KAMPALA, Uganda.
NJEMBA mmoja amekutwa na rundo la kondomu tumboni mwake.
Mtu huyo alikamatwa akiwa na dawa za kulevya aina ya nikotini tumboni mwake zikiwa ndani ya mipira ya kondomu.

Kwa sasa yupo chini ya ulinzi mkali wa polisi nchini Uganda, ambapo madaktari wanajaribu kuz
itoa tumboni.

Mtuhumiwa huyo ambaye ni raia wa Guinea, alitiwa mbaroni hivi karibuni. Tayari madaktari wameshamtoa kondomu takriban 21 zenye dawa kwa njia ya kutapika na haja kubwa.

“Mtu huyo alitapika kondomu 20 na baada ya kupewa dawa aina ya Bisacodyl alitoa kondomu nyingine moja kwa njia ya choo,” alisema daktari mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa si msemaji.

Daktari huyo alisema anasikitika kuwa utaratibu wa kumtoa dawa hizo unachukuwa muda mrefu na kueleza kwamba acidi zinazomtoka mwilini zinaweza kudhoofisha mipira hiyo na kupasukia tumboni hivyo kuhatarisha maisha yake.

“Licha ya kumfanyia vipimo kadhaa, tumeshindwa kumfanyia upasuaji kwani hatujabaini ni wapi hasa mipira hiyo ilipo,” alisema daktari huyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI