BARCELONA NDEMBE-NDEMBE, BAYERN HIYOO FAINALI ULAYA

 Dimba la Nou Camp dakika chache kabla ya kuanza kwa pambano la marudiano, nusu fainali Mabingwa Ulaya kati ya wenyeji FC Barcelona, dhidi ya FC Bayern Munich ya Ujerumani. Katika mechi hiyo, Bayern ilishinda kwa mabao 3-0 na kufuzu fainali huku ikiitoa Barca kwa jumla ya mabao 7-0 baada ya kushinda 4-0 katika mechi ya kwanza wiki iliyopita huko Allianz Arena jijini Munich Ujerumani.
 Bao la kwanza la Bayern likitinga nyavuni. Bao hilo lilifungwa na Mholanzi Arjen Robben (hayupo pichani).
 Wachezaji wa Bayern wakitoka kumpongeza Robben (wa pili kulia), baada ya kuifungia bao hilo la uongozi.
 Robben (mwenye upara) akipongezwa na nyota wenzake wa Bayern Munich.
 Mwanasoka Bora wa Dunia kwa mwaka wa nne mfululizo, Lionel Messi (kulia), akiwa aamini macho yake baada ya Barca kukubali kufungwa bao la kwanza, lililomaanisha ongezeko la mlima inaopasa kuupanda timu yake kuelekea Wembley inakopigwa fainali ya Ulaya wiki tatu zijazo.
 Beki wa Barcelona, Gerard Pique (katikati) akijifunga bao langoni kwake na kuiandikia Bayern bao la pili katika mechi hiyo.
 Thomas Muller wa Bayern (25) akipiga kichwa kuipa timu yake bao la tatu na la ushindi dhidi ya Barca.
 Andres Iniesta wa Barca akifumua shuti kujaribu kuifungia timu yake katika mtanange huo.
 Kipa wa Bayern, Manuel Neuer akipangua moja ya hatari langoni kwake.
 Nyota wa Bayern, Arjen Robben, akizungumza jambo na kocha wake Jupp Heyneckes
 Pique akiteta jambo na David Villa na Cesc Fabregas wakati wa mtifuano huo.
 Mtokea benchi Marc Bartra wa Barcelona, akianguka chini baada ya kushindwa mchuano wake na mshambuliaji Mario Mandzukic wa Bayern.
 Beki wa Barca, Gerard Pique akitafuta mbinu za kumtibulia kiungo Bastian Schweinsteiger wa Bayern anayemiliki mpira.
Hapa kipa wa Barca, Victor Valdes alikuwa akimlaumu Pique kwa kujifunga 'kujitia nyama' mwenyewe.
 Wachezaji wa Bayern wakiwa wamevalia fulana maalum za fainali ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Wembley, jijini London, Jumamosi Mei 25.
Robben na Schweinsteiger wa Bayern, wakiwa na furaha ya ushindi uliowapeleka fainali wanakotarajia kuumana na Wajerumani wenzao Borussia Dortmund iliyoing'oa Real Madrid.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA